Mtaalam wa Ethiopia asema hatua ya nchi hiyo kujiunga na BRICS itasaidia kuinua uchumi wa nchi hiyo

(CRI Online) Agosti 28, 2023

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Huduma za Jamii nchini Ethiopia Mukerrim Miftah amesema, hatua ya nchi hiyo kujiunga na BRICS inatarajiwa kuchochea kidhahiri ukuaji wa uchumi na kuimarisha manufaa yake ya kunufaishana ya kikanda.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Miftah amesema hatua hii ni ya msingi kwa sababu kadhaa, ikiwemo kuisaidia Ethiopia kujenga ushirikiano wa nguvu wa kiuchumi na kisiasa na nchi wanachama wa BRICS, kusaidia uhusiano mzuri wa uchumi, biashara na uwekezaji kati yake na nchi mpya na zile zilizopo katika kundi la BRICS.

Amesisitiza kuwa uanachama wa Ethiopia katika BRICS utawezesha nchi hiyo kuendeleza uhusiano wa kigeni katika njia ya kitaasisi zaidi na ya kunufaishana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha