

Lugha Nyingine
Mtaalam asema Ushirikiano wa dhati kati ya Afrika na China unaleta manufaa yanayoonekana na maendeleo kwa pamoja
LUANDA - Ushirikiano wa dhati wa China na nchi za Afrika unazaa "matunda yanayoonekana na ya kuhimiza juhudi" ambayo yanaleta manufaa ya pande zote na maendeleo kwa pamoja, amesema mtaalam wa Angola.
Kwenye ushirikiano kati yake na Afrika, China imeweka msingi muhimu wa miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika bara zima, na hivyo kuleta ukuaji wa viwanda na kuongeza thamani ya kibiashara ya bara la Afrika, amesema Osvaldo Mboco, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Angola katika mahojiano yake kwa njia ya maandishi na Shirika la Habari la China, Xinhua kufuatia Mazungumzo ya Viongozi Wakuu wa China na Afrika yaliyofanyika Alhamisi nchini Afrika Kusini.
"Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa mshirika mkuu wa kiuchumi na kifedha kwa nchi za Afrika. Zaidi ya kuweka mifumo ya miundombinu, nchi hiyo inaliona Bara la Afrika kama soko la biashara lenye kujaa matumaini zaidi kuliko mchango wake wa kuchukuliwa kama chanzo cha malighafi." Mboco amesema.
Angola sasa imeibuka kuwa soko muhimu barani Afrika, inashuhudia kampuni nyingi zaidi za China zinazoanzisha au kupanga kuanzisha vituo vya uzalishaji wa viwandani na mistari ya kuunganisha na kukamilisha sehemu za bidhaa, amesema mtaalam huyo, huku akiongeza kuwa kampuni hizi za China zinasaidia kutoa nafasi za ajira kwa wenyeji wa Angola.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ubalozi wa China nchini Angola, katika miaka ya hivi karibuni, kampuni za China, kwa kukarabati au kujenga reli yenye urefu wa kilomita 2,800, barabara zenye urefu wa kilomita 20,000, shule zaidi ya 100, hospitali 50, na nyumba za makazi zaidi ya 100,000, zimechangia Angola kupiga hatua ya maendeleo.
Bidhaa za China zinakaribishwa katika soko la Angola, na kuleta faida za biashara na uwekezaji za kunufaishana kwa nchi hizo mbili.
Kuhusu mwelekeo unaowezekana wa ushirikiano kati ya China na Afrika, Mboco anatarajia njia moja ya kuelekea maendeleo ya teknolojia ya hali ya juu, hasa anafuatilia zaidi maeneo muhimu kama vile akili bandia, teknolojia ya anga ya juu na nyanja zinazohusika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma