Viongozi wa Misri na Sudan wajadili uhusiano na mgogoro wa Sudan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2023

Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi (Kulia) akipeana mkono na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, ambaye pia ni Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Sudan, mjini New Alamein, Misri, Agosti 29, 2023. (Ikulu ya Misri / Xinhua)

CAIRO - Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan wamejadili uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya hivi karibuni katika mgogoro wa Sudan siku ya Jumanne.

Msemaji wa Ikulu ya Misri amesema katika taarifa yake kwamba kwenye mkutano huo uliofanyika mji wa pwani wa New Alamein, Sisi ametilia maanani sana ukaribu wa kihistoria na uhusiano wa pande zote kati ya nchi yake na Sudan kwenye ngazi ya serikali rasmi na kati ya watu.

Taarifa hiyo imesema, sisi pia amesisitiza msimamo thabiti wa Misri kushikamana na Sudan na kuunga mkono usalama, utulivu, umoja na ukamilifu wa eneo lake, hasa wakati wa hali mbaya ya sasa.

Kwa upande wake, Al-Burhan, ambaye pia ni Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Sudan, ameishukuru Misri kwa kuunga mkono usalama na utulivu wa Sudan katika "wakati wa kihistoria inaopitia," hasa kuwakaribisha raia wa Sudan.

Kwenye mkutano huo, viongozi hao wawili pia walikumbuka maendeleo ya Sudan na kugusia njia za kuhakikisha msaada wa kibinadamu kwa watu wa Sudan na juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan.

Pia wamezungumzia utaratibu wa kutatua mgogoro uliopendekezwa katika mkutano kati ya nchi jirani, ambao ulifanyika katikati ya Julai katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi (Kulia) akikutana na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, ambaye pia ni Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Sudan, mjini New Alamein, Misri, Agosti 29, 2023. (Ikulu ya Misri / Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha