China yapandisha hatua ya dharura ya ngazi ya IV dhidi ya mafuriko katika maeneo ya kusini mwa nchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2023

Wafanyakazi wakijaribu kutiririsha na kuvujisha maji ya mafuriko katika maeneo ya mjini Qinzhou katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Julai 18, 2023. (Xinhua/Zhang Ailin)

Wafanyakazi wakijaribu kutiririsha na kuvujisha maji ya mafuriko katika maeneo ya mjini Qinzhou katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China, Julai 18, 2023. (Xinhua/Zhang Ailin)

Beijing - Wizara ya Maji ya China Jumatano imepandisha mwitikio wa dharura wa ngazi ya IV kwa kukabiliana na mafuriko katika maeneo sita ya ngazi ya mikoa, Kusini mwa China.

Mikoa ya Fujian, Jiangxi, Hunan, Guangdong, Guangxi na Hainan imeitikia hatua za dharura, wizara hiyo imesema. Pia imetuma vikundi kazi viwili huko Fujian na Guangdong kusaidia kuzuia mafuriko.

Kimbunga Saola, ambacho ni kimbunga cha tisa kuikumba China mwaka huu, kinatazamiwa kuleta mvua kubwa katika maeneo mengi ya Kusini mwa China kuanzia leo Alhamisi hadi Jumamosi, wizara hiyo imesema. Viwango vya maji katika baadhi ya mito katika maeneo ya mtiririko wa Mto Zhujiang, Mto Changjiang na Ziwa Taihu vitapanda huku vikileta hatari ya mafuriko.

Kituo cha Taifa cha Hali ya Hewa cha China kimesema kuwa kimbunga hicho kinaweza kutua mahali fulani kwenye pwani ya China ndani ya eneo linaloanzia Mashariki mwa Mkoa wa Guangdong hadi Kusini mwa Mkoa wa Fujian wakati wa mchana siku ya Ijumaa, au kinaweza kuelekea kusini-magharibi kutoka pwani ya mashariki ya Guangdong. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha