Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi afanya mazungumzo na mwenzake wa Uingereza James Cleverly

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akifanya mazungumzo na James Cleverly, Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo wa Uingereza hapa Beijing, China, Agosti 30, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na James Cleverly, Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo wa Uingereza, mjini Beijing siku ya Jumatano.

Kwenye mazungumzo hayo, Wang, amesema China siku zote imekuwa ikiweka umuhumi kwenye hadhi ya Uingereza kama nchi yenye nguvu kubwa na mchango wake wa kipekee, imejitolea kudumisha uhusiano thabiti na wa kunufaishana kati ya China na Uingereza na siku zote inaamini kuwa ushirikiano kati ya China na Uingereza una ushawishi duniani.

Huku akisisitiza kuwa mazungumzo na ushirikiano ndiyo maneno muhimu na sauti kuu ya sera ya China kuhusu Uingereza, Wang amesema wakati dunia inapokabiliwa na mabadiliko na changamoto kubwa, China na Uingereza zikiwa nchi kubwa zinapaswa kuonyesha wajibu wao ili kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za kimataifa na kulinda amani na utulivu wa Dunia, na kusukuma mbele uhusiano kati ya China na Uingereza badala ya kurudi nyuma.

Wang ameeleza msimamo wa China kuhusu suala la Taiwan, akisisitiza kwamba "kujitenga kwa Taiwan" hakuendani na utulivu katika eneo la Mlango-Bahari wa Taiwan, na Uingereza inapaswa kuheshimu kwa dhati maslahi makuu ya China na kufuata sera ya kuwepo kwa China moja.

Kwa upande wake Cleverly amesema uhusiano mzuri kati ya Uingereza na China utanufaisha watu na Dunia. Na msimamo wa serikali ya Uingereza kuhusu suala la Taiwan bado haujabadilika. Serikali ya Uingereza inafuata sera ya kuwepo kwa China moja.

Cleverly amesema, Uingereza imejitolea kuimarisha mawasiliano na China, inafanya juhudi za kuchukua hatua za kutatua matatizo, kuongeza kuelewana, na kukumbatia fursa, na ameongeza kuwa kampuni za biashara za Uingereza zinatarajia ushirikiano zaidi na China na kutafuta fursa za soko la China.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu mgogoro wa Ukraine na suala la nyuklia la Peninsula ya Korea. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akifanya mazungumzo na James Cleverly, Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo wa Uingereza hapa Beijing, China, Agosti 30, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akifanya mazungumzo na James Cleverly, Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo wa Uingereza hapa Beijing, China, Agosti 30, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha