Balozi wa China nchini Marekani aonya dhidi ya kutengana kiuchumi na mgogoro kati ya China na Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2023

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng akizungumza kwenye mkutano wa kifungua kinywa ulioandaliwa na Shirikisho la Teknolojia ya Hali ya Juu ya Afya (AdvaMed) kwa mwaliko huko Washington, D.C., Marekani, Juni 28, 2023. (Xinhua/Liu Jie)

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng akizungumza kwenye mkutano wa kifungua kinywa ulioandaliwa na Shirikisho la Teknolojia ya Hali ya Juu ya Afya (AdvaMed) kwa mwaliko huko Washington, D.C., Marekani, Juni 28, 2023. (Xinhua/Liu Jie)

WASHINGTON - Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng ameonya dhidi ya kutengana kiuchumi na mgogoro kati ya China na Marekani kwenye hotuba aliyoitoa katika kongamano la kibiashara huko Washington, D.C., Marekani.

Akihutubia baraza la tano la Biashara kati ya Marekani na China lililoandaliwa na Jarida la Forbes, balozi Xie amesema hatari kubwa zaidi ni kujitenga kiuchumi kati ya China na Marekani, na chanzo kikubwa zaidi cha hali ya ukosefu wa usalama kinatokana na mapambano kati ya nchi hizo mbili.

Mgororo au mapambano yoyote kati ya China na Merika hayatatoa mshindi, lakini tu kutasababisha maafa kwa Dunia, Xie amesema, huku akiongeza kuwa chaguo sahihi pekee kwa nchi hizo mbili ni kukabiliana na changamoto za kimataifa kwa pamoja, na kutoa faida zaidi za amani na maendeleo kwa Dunia.

Akijibu sauti zilizoibuka hivi karibuni kuhusu kudidimia kwa uchumi wa China, Balozi Xie amesema sauti hizo hazitafanya mtu yeyote kuwa bora zaidi, na Dunia itakuwa ustawi zaidi kutokana na China kuendelezwa vizuri.

Balozi Xie amesema kuwa marafiki kutoka jumuiya ya wafanyabiashara ni "washikadau" muhimu katika uhusiano kati ya China na Marekani. Amewahimiza kuendelea kujenga madaraja ya urafiki na ushirikiano na kuchukua jukumu muhimu katika kuimarisha mabadilishano ya pande mbili na kuleta utulivu katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Balozi Xie amesema moja ya kazi zake muhimu ni kutafuta wafuasi wa uhusiano kati ya China na Marekani, kupunguza tofauti na kutoelewana, kupanua mazungumzo na ushirikiano ili kuufanya uhusiano kati ya China na Marekani urejee kwenye njia sahihi na kusonga mbele.

"Kwa kutazama mbele, tunahitaji kuendelea kuchukua hatua madhubuti, haijalishi ni ndogo kiasi gani," Balozi Xie amesema, huku akipendekeza kwamba pande hizo mbili zinapaswa kutafuta matokeo ya ushirikiano yanayoonekana na kuingiza nishati chanya zaidi katika uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kwa mfano, kwa kurekebisha ushauri wa Wamarekani kusafiri China, kurejesha makubaliano katika ushirikiano wa sayansi na teknolojia kati ya China na Marekani, kufanya Mkutano wa Kilele wa Uongozi wa Utalii wa China na Marekani, na kuwezesha maombi ya visa na kuvuka mpaka kwa raia wa kila upande.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha