China yasema kuongeza wanachama katika kundi la BRICS kutaongeza sauti ya nchi zinazoendelea kwenye mambo ya kimataifa

(CRI Online) Agosti 31, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, kuongeza wanachama katika ushirikiano wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) kutaongeza sauti ya nchi zenye masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea kwenye masuala ya kimataifa.

Akizungumza Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bw. Wang amesisitiza kuwa, lengo la ushirikiano wa BRICS ni kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja, hautajihusisha na mvutano kati ya makundi mbalimbali, na ushirikiano wa BRICS ni tofauti kimsingi na kundi dogo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha