China yaitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono zaidi maendeleo ya vijana barani Afrika

(CRI Online) Agosti 31, 2023

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing, amesema China imejikita katika kulinda amani na maendeleo ya Afrika, kuchukua hatua za kivitendo kuunga mkono maendeleo ya vijana barani Afrika, na pia iko tayari kushirikiana na jamii ya kimataifa kuunga mkono zaidi vijana wa bara hilo.

Balozi Dai amesema, hivi sasa baadhi ya nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za vita, ugaidi na usalama wa chakula, na kundi lililo hatarini zaidi ni vijana.

Amesema hivi karibuni China imetangaza kuanzisha Mpango wa Kuunga Mkono Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika”, kutekeleza “Mpango wa China Kusaidia Maendeleo ya Kilimo cha Kisasa Barani Afrika”, na “Mpango wa Kuwaandaa kwa Pamoja Wataalamu wa China na Afrika.”

Amesema, hatua hizo zinaendana na mahitaji ya sasa ya Afrika, na kusaidia maendeleo ya vijana barani humo kwa hatua za kivitendo.

Pia amesema hatua za China za kuunga mkono zaidi vijana wa Afrika ni pamoja na kuonesha umuhimu wa vijana katika kuhimiza ufumbuzi wa kisiasa wa masuala yanayofuatiliwa, kuzuia mapigano ya kutumia silaha na kupunguza hatari za mapigano hayo kwa vijana, pamoja na kuhimiza amani kwa maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha