China yatoa wito wa kulindwa utaratibu wa kimataifa wa usalimishaji wa silaha

(CRI Online) Agosti 31, 2023

Mjumbe wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Ren Hongyan ametoa wito wa kudumishwa kwa utaratibu wa kimataifa wa usalimishaji wa silaha na kupinga mawazo ya vita baridi na mivutano ya kambi.

Akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha "Siku ya Kimataifa ya Kupiga Marufuku Majaribio ya Nyuklia", Balozi Ren amesema, mfumo wa kimataifa wa udhibiti, usalimishaji na kutoeneza silaha unakabiliwa na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa, na hatari za mashindano ya silaha za nyuklia na migogoro ya nyuklia zinaongezeka mara kwa mara.

Amesema kutokana na hali hii, ni lazima kutekeleza kwa uthabiti ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, na kushikilia taratibu za kimataifa za usalimishaji wa silaha, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Kupiga Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia, kupinga mawazo ya Vita Baridi na mivutano ya kambi, na kufanya jitihada zaidi katika kutilia maanani ustawi wa binadamu wote na kufikia usalama wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha