

Lugha Nyingine
China yadumisha viwango vya tahadhari dhidi ya mafuriko na kimbunga katika mikoa ya kusini
Picha hii iliyopigwa Septemba 2, 2023 ikionyesha mti ulioanguka kando ya barabara ya Shennan huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Liang Xu)
BEIJING - Makao Makuu ya Kitaifa ya Kuzuia Mafuriko na Kupambana na Ukame ya China yamefanya uamuzi wa kuendelea na hatua ya dharura ya Ngazi ya III kwa kukabiliana na mafuriko na vimbunga katika Mikoa ya Fujian na Guangdong, pamoja na mwitikio wa Ngazi ya IV katika Mikoa ya Zhejiang, Guangxi na Hainan.
Kimbunga Saola, ambacho ni kimbunga cha tisa kuikumba China kwa mwaka huu, kinaelekea katika Ghuba ya Beibu katika Bahari ya China Kusini baada ya kutua katika Mji wa Zhuhai huko Guangdong Jumamosi alasiri.
Habari zimesema, kimbunga Haikui, ambacho ni kimbunga cha 11 kuikumba China kwa mwaka huu, kimetua kwenye Kisiwa cha Taiwan na kuleta mvua kubwa Jumapili jioni, na kinakadiriwa kuweza kuleta upepo na mvua kubwa katika Mikoa ya Fujian na Guangdong.
Mikoa ya Fujian, Guangdong na Zhejiang imeshauriwa kuchukua tahadhari dhidi ya Kimbunga Haikui na mvua zinazoendelea kunyesha.
Makao makuu yametuma vikundi kazi katika mikoa hiyo mitatu kusaidia katika maandalizi yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma