

Lugha Nyingine
Madaktari wa Namibia wajifunza Matibabu ya Jadi ya China ili kusaidia jamii za wenyeji
Mtaalamu wa Dawa za Mitishamba za Kichina (TCM) Wang Peng (Kulia) akijadili matibabu ya mgonjwa na madaktari wawili wa mafunzo kwa vitendo huko Windhoek, Namibia Agosti 31, 2023. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)
WINDHOEK - Katika mwaka mmoja na nusu uliopita, Tileinge Hapulile, kama ilivyo kwa wataalamu wengine wengi wa tiba nchini Nambia, amekuwa akijifunza matibabu ya jadi ya China (TMC) kusaidia wagonjwa katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.
Hapulile alitambulishwa kwa Wang Peng, aliyekuwa daktari wa timu ya madaktari wa China nchini Namibia aliyebobea katika matibabu ya jadi ya China ambaye sasa anaendesha kliniki katika mji mkuu, Windhoek, na kujuana kwao huko kuliamsha shauku ya Hapulile katika matibabu ya jadi ya China kutokana na kuvutiwa na matibabu ya jadi ya China na desturi ya familia yake ya kutegemea dawa za mitishamba.
"Nimeona tofauti kati ya matibabu ya jadi ya China na ya Magharibi. Nadhani matokeo ya michanganyiko hiyo miwili ni makubwa," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.
Hapulile na Wang wanahudumia wagonjwa 17 hadi 20 kila siku katika zahanati hiyo wakilenga maumivu ya goti, kiuno na bega kwa kutumia matibabu mbalimbali ya jadi ya China kama vile Tuina.
"Matokeo yamekuwa mazuri kwa kiasi kikubwa, tangu mwaka wangu wa kwanza hadi sasa, tumeshuhudia ongezeko la wagonjwa kutokana na matokeo mazuri," ameongeza.
Kijana huyo wa Namibia ameondoka kwenda China Jumapili kusomea shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Matibabu ya jadi ya China cha Zhejiang katika mji wa Hangzhou, Mashariki mwa China.
“Nataka kutumia ujuzi na utaalamu wangu nilioupata kusaidia wagonjwa wengi zaidi kwa sababu hivi sasa kuna madaktari bingwa wapatao watatu pekee wenye utaalam wa matibabu ya jadi ya China wakiwemo wale wa zahanati ya Wachina iliyopo Hospitali ya Katutura,” amesema.
Huku matibabu ya jadi ya China yakizidi kupendwa miongoni mwa watu huko Windhoek, wataalamu wengi wa matibabu kama Hapulile wanaanza kufanya mazoezi ya matibabu hayo. Katika kliniki ya Wang, Sten Shinyemba, daktari mhitimu wa shahada ya kwanza ambaye aliwahi kusoma katika Chuo Kikuu cha Hebei Kaskazini katika Mkoa wa Hebei, Kaskazini-Magharibi mwa China, amekuwa akiendeleza maarifa na ujuzi wake katika matibabu ya jadi ya China kwa miezi sita.
“Kwa kweli niliamka siku moja ndipo nilipogundua kuwa ni ndoto ambayo nilitaka kuifanya, kwa sababu nilisoma matibabu ya jadi ya China kama somo katika mitaala yetu ya chuo kikuu, na ilikuwa ya kuvutia sana,” amesema.
Shinyemba amesema matibabu ya jadi ya China yameonyesha matokeo mazuri kwa wagonjwa wake.
Daktari mwenyeji wa Namibia Tileinge Hapulile anayefanya mazoezi akitoa matibabu ya acupuncture huko Windhoek, Namibia Agosti 31, 2023. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma