China na Indonesia zachangia maono sawa na maslahi ya pamoja: Waziri Mkuu wa China Li Qiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2023

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza kwenye hafla ya ukaribisho iliyoandaliwa na jumuiya ya wafanyabiashara wa China na Indonesia mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Rao Aimin)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akizungumza kwenye hafla ya ukaribisho iliyoandaliwa na jumuiya ya wafanyabiashara wa China na Indonesia mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Rao Aimin)

JAKARTA - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema kwamba China na Indonesia zinachangia maono yanayofanana, maafikiano mapana na maslahi ya pamoja katika ngazi za kikanda na kimataifa.

Katika hotuba yake aliyoitoa Jumanne kwenye hafla ya ukaribisho iliyoandaliwa na jumuiya ya wafanyabiashara wa China na Indonesia, Waziri Mkuu Li amesema kwa muda mrefu, ushirikiano kati ya China na Indonesia umevuka upeo wa nchi mbili, na kuongeza kuwa zote mbili ni nchi zinazoibukia zenye nia kubwa ya ustawishaji wa taifa, na zote mbili zimejitolea kudumisha uwazi, ujumuishaji, mapatano na utulivu katika kanda.

Akibainisha kuwa ziara yake hiyo ni ya kwanza kwake katika nchi ya Asia tangu awe Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China, Waziri Mkuu Li amesema kuifanya Indonesia kuwa kituo chake cha kwanza cha ziara hiyo ni kwa ajili ya maendeleo, urafiki, amani na ushirikiano, na kuongeza kuwa China na Indonesia ni majirani wema, ndugu wema na washirika wema, na uhusiano wa kirafiki kati yao unaodumu kwa muda mrefu unaendelea kung'aa.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni, chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Indonesia umepata maendeleo makubwa, na kuleta manufaa halisi kwa watu wa pande hizo mbili.

“Nchi hizo mbili ni washirika muhimu wa kibiashara wa upande mwingine, ushirikiano wa uwekezaji kati ya nchi hizo mbili umekua kwa kuleta manufaa na faida kubwa na minyororo yao ya viwanda na ugavi imeunganishwa kwa pande zote, na kufikia mafanikio ya pande zote,” amesema Waziri Mkuu Li.

Huku ikisisitiza kuwa China itaongeza kasi ya ufunguaji mlango, kupanua zaidi upatikanaji wa soko katika maeneo kama vile ya huduma za kisasa, na kufanya juhudi zaidi kulinda haki miliki, Waziri Mkuu Li amesema, China itafanya jitihada za kuweka mazingira ya biashara yenye kiwango cha kimataifa, yenye mwelekeo wa soko yanayoongozwa na mfumo mzuri wa kisheria huku akitumai kuwa Indonesia itaendelea kufanya soko lake kuwa wazi na kutoa mazingira ya haki na ya usawa ya kibiashara kwa kampuni za China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha