

Lugha Nyingine
Mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya Asia ya Hangzhou kuanza Septemba 8 karibu na Ziwa Xihu
![]() |
Mkutano na waandishi wa habari wa mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya 19 ya Asia ya Hangzhou ukifanyika kwenye Kituo Kikuu cha Habari cha Michezo ya Asia ya Hangzhou, huko Hangzhou, China, Septemba 6, 2023. (Xinhua/Jiang Han) |
HANGZHOU - Mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya Asia ya Hangzhou zimepangwa kuanza Septemba 8 karibu na Ziwa Xihu, waandaaji wa michezo hiyo wametangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatano uliofanyika Kituo Kikuu cha Vyombo vya Habari cha michezo hiyo ya Asia itakayofanyika katika Mji wa Hangzhou ulioko Mkoa wa Zhejiang, China.
Mwenge huo utapita katika miji 11 katika Mkoa wa Zhejiang, ikijumuisha Huzhou, Jiaxing, Shaoxing, Ningbo, Zhoushan, Taizhou, Wenzhou, Lishui, Jinhua na Quzhou, kabla ya kurejea Hangzhou Septemba 20 kukamilisha kituo chake cha mwisho.
Jumla ya wakimbiza mwenge 2,022 watashiriki katika mbio hizo za kupokezana mwenge, wakiwa na umri wa kuanzia miaka 14 hadi 84.
Kwa kuendana na moyo wa michezo hiyo ya kuwa ya "kijani, teknolojia za kisasa, kiuchumi na maadili," upangaji wa njia ya mbio hizo za kupokezana mwenge wa Michezo ya Asia ya Hangzhou unasisitiza urahisi na kufaa. Muundo wa njia za mbio hizo katika kila eneo unaonyesha umaalumu wa kila sehemu, umuhimu wa kihistoria na kitamaduni, na mandhari ya miji husika, na kuhakikisha uanuai wa mbio na kuwa zenye mandhari ya kuvutia.
Zaidi ya hayo, mbio hizo unafanyika mtandaoni na nje ya mtandao. Kufuatia Hafla ya Kuwasha Moto wa Mwenge wa Michezo ya Asia Juni 15, shughuli ya "Wakimbiza Mwenge Kidijitali" kupokezana mtandaoni ilizinduliwa. Hadi sasa, idadi ya "Wakimbiza Mwenge Kidijitali" imezidi watu milioni 84.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma