Waziri Mkuu wa China Li Qiang asema uhusiano kati ya China na Cambodia ni thabiti na kuweka mfano kwa aina mpya ya uhusiano wa kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2023

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet  katika wakati wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 6, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

JAKARTA - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Waziri Mkuu mpya wa Cambodia Hun Manet, akisema kuwa uhusiano wa nchi hizo mbili umehimili mabadiliko katika hali ya kimataifa, na umeendelea kuwa mwamba mgumu na usioweza kuvunjika, na kuweka mfano kwa aina mpya ya uhusiano wa kimataifa.

Viongozi hao wawili wa serikali wamekutana siku ya Jumanne katika wakati wa mikutano ya viongozi wa ushirikiano wa Asia Mashariki iliyofanyika mjini Jakarta, Indonesia, ambayo ni Mkutano wa 26 wa Kilele wa China na ASEAN, Mkutano wa 26 wa Kilele wa ASEAN+3 na Mkutano wa 18 wa Kilele wa Asia Mashariki. Na hii ni mara ya kwanza kukutana kwa mawaziri hao wawili.

“China imekuwa mshirika wa kutegemewa wa Cambodia, na kama kawaida, itaiunga mkono Cambodia kwa uthabiti katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi yake, na katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo,” Waziri Mkuu Li amesema.

Ametoa wito kwa pande hizo mbili kuimarisha mawasiliano ya kirafiki, kufungamanisha zaidi mikakati yao ya maendeleo na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

Waziri Mkuu Li pia ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuchukua fursa ya mazungumzo kuhusu kusaini mpango mpya wa utekelezaji wa ujenzi wa jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja , na kufanya mipango ya pande zote ya ushirikiano wa kimkakati wa pande hizo mbili, ili kuchangia ustawi, maendeleo na utulivu wa muda mrefu wa Cambodia.

Amesema kwamba, pande zote mbili zinapaswa, kuendelea kufanya kazi pamoja ili kulinda msingi mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) na kuweka ushirikiano wa kikanda kwenye mwelekeo sahihi.

Kwa upande wake Hun Manet amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili miaka 65 iliyopita, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa wenye matunda, na China imekuwa rafiki na mshirika mzuri wa kutegemewa wa Cambodia.

Amesema serikali mpya ya Cambodia itaendelea kufuata kanuni na mfumo wa uhusiano wa Cambodia na China, na kufanya kazi pamoja na upande wa China katika kusukuma maendeleo mapya ya ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta zote kwenye msingi wa uhusiano wa kirafiki wa nchi hizo mbili uliojengwa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Cambodia Samdech Techo Hun Sen na Rais wa China Xi Jinping. 

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet  katika wakati wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 6, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet katika wakati wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 6, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha