Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aonya "kushindwa kuhimili kwa Tabianchi kumeanza"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2023

Watu wakijipoza joto la mwili chini ya kituo cha kupoza joto la mwili kwa maji ya kunyunyizia kwenye Bustani ya Wanyama ya Smithsonian huko Washington, D.C., Marekani, Julai 26, 2023. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)

Watu wakijipoza joto la mwili chini ya kituo cha kupoza joto la mwili kwa maji ya kunyunyizia kwenye Bustani ya Wanyama ya Smithsonian huko Washington, D.C., Marekani, Julai 26, 2023. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya Jumatano kwamba "kushindwa kuhimili kwa tabianchi kumeanza."

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa yenye maneno makali juu ya rekodi ya joto kali duniani katika majira ya joto katika Dunia ya Kaskazini, kwa mujibu wa shirika la huduma ya hali ya hewa la Umoja wa Ulaya, Copernicus na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

"Siku za mbwa (siku joto katika lugha ya Kiingereza) za majira ya joto siyo tu zinabweka, zinang’ata," Guterres amesema, huku akiongeza kuwa "sayari yetu imestahimili msimu wa kuungua - majira ya joto yenye hali joto kali zaidi katika rekodi. Kushindwa kuhimili kwa tabianchi kumeanza."

Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa "wanasayansi wameonya kwa muda mrefu kile ambacho uraibu wetu wa kutumia nishati ya makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia utasababisha nini."

"Tabianchi yetu inalipuka kwa kasi zaidi kuliko tunavyoweza kukabiliana na matukio mabaya ya hali ya hewa yanayokumba kila kona ya sayari."

"Kuongezeka kwa joto kunahitaji kuongezeka kwa hatua," Guterres amesema.

Ametoa wito kwa viongozi "kuongeza joto sasa kwa suluhisho la tabianchi."

"Bado tunaweza kuepuka machafuko mabaya zaidi ya tabianchi - na hatuna muda wa kupoteza," amesema.

Dunia imetanda katika majira ya joto yenye hali joto kali zaidi katika Dunia ya Kaskazini kuwahi kurekodiwa, huku rekodi ya joto katika Mwezi Agosti ikijumuisha msimu wa joto kali na lenye maafa, kwa mujibu wa WMO.

Mwezi uliopita haukuwa tu mwezi wa Agosti wenye joto kali kuwahi kurekodiwa kwa vifaa vya kisasa, pia ulikuwa mwezi wa pili kwa kuwa na joto kali zaidi lililorekodiwa, nyuma ya Julai 2023 tu, WMO na Copernicus zimetangaza Jumatano. 

Binti mdogo akipoza joto la mwili kwenye chemchemi ya Three Graces liyopo Place de Comedie wakati ambapo halijoto ya juu zaidi ilipofikia nyuzi joto 38 huko Montpellier, Kusini mwa Ufaransa, Julai 19, 2023. (Xinhua/Gao Jing)

Binti mdogo akipoza joto la mwili kwenye chemchemi ya Three Graces iliyopo Place de Comedie wakati ambapo halijoto ya juu zaidi ilipofikia nyuzi joto 38 huko Montpellier, Kusini mwa Ufaransa, Julai 19, 2023. (Xinhua/Gao Jing)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha