

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China Li Qiang atoa wito wa kutoingiza siasa katika masuala ya kiuchumi
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika wakati wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Kusini Mashariki mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 7, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)
JAKARTA - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema kwamba Dunia inapaswa kupinga kwa pamoja kuongeza kupita kiasi maana ya usalama na kuingiza siasa katika masuala ya kiuchumi.
Waziri Mkuu Li ameyasema hayo siku ya Alhamisi alipokutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres katika wakati wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Kusini Mashariki iliyofanyika mjini Jakarta, ambayo ni Mkutano wa 26 wa Kilele wa China na ASEAN, Mkutano wa 26 wa Kilele wa ASEAN+3 na Mkutano wa 18 wa Kilele wa Asia Mashariki.
“Mazingira ya sasa ya kimataifa yamegubikwa na mabadiliko na machafuko, na kadiri hali inavyozidi kuwa mbaya, ndivyo jumuiya ya kimataifa inavyohitaji kuungana na kushirikiana ili kukabiliana na changamoto,” amesema Waziri Mkuu wa China.
Amesisitiza kuwa ni muhimu kuharakisha mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa uchumi wa dunia na kuongeza ipasavyo uwakilishi na sauti ya nchi zinazoendelea katika taasisi za fedha za kimataifa.
Ameitaka jumuiya ya kimataifa kushughulikia kwa makini suala la madeni ya nchi zinazoendelea kwa kufuata kanuni ya hatua za pamoja na kuchangia mzigo kwa haki.
Waziri mkuu Li alipotoa wito wa kushikilia mifumo inayoongozwa na Umoja wa Mataifa ili kuendeleza ushirikiano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi alisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu mapendekezo aliyotoa Rais Xi Jinping wa China kuhusu kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja na “Ukanda Mmoja, Njia Moja” .
“Katika miaka ya hivi karibuni, Rais wa China kwa mfululizo ametoa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia, na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, kutoa ufumbuzi wa China kwa maendeleo na usimamizi wa Dunia ” Waziri Mkuu Li amesema.
Kwa upande wake Guterres amesema, kutokana na changamoto mbalimbali, nchi zote zinapaswa kuungana kuwa kitu kimoja, kuimarisha hali ya kuaminiana, kuzuia kugawanyika kwa uchumi wa Dunia, na kukabiliana kwa pamoja na changamoto za kimataifa.
Akibainisha kuwa China inafanya kazi yake muhimu katika kuendeleza ajenda ya kimataifa, Gutteres amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kuimarisha mazungumzo na ushirikiano na China, kuhimiza mageuzi ya mfumo wa kushughulikia uchumi wa kimataifa, na kuzisaidia nchi zinazoendelea kupata raslimali za kutosha kwa kukabiliana na changamoto za usalama wa chakula, afya ya umma na mabadiliko ya tabia nchi, ili kutoa mchango kwa ajili ya kutekeleza kihalisi Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika wakati wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Kusini Mashariki mjini Jakarta, Indonesia, Septemba 7, 2023. (Xinhua/Zhang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma