Chombo cha kubeba mizigo kwenye anga ya juu cha China, Tianzhou-5 chatengana na muunganiko wa kituo cha anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 12, 2023

Picha hii ya mfano iliyopigwa kwenye Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing, Novemba 12, 2022 ikionyesha chombo cha kubeba mizigo kwenye anga ya juu cha China, Tianzhou-5 kikiwa kimetekeleza minyumbuliko ya kiotomatiki na kutia nanga na muunganiko wa kituo cha anga ya juu cha China, Tiangong. (Picha na Sun Fengxiao/Xinhua)

Picha hii ya mfano iliyopigwa kwenye Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing, Novemba 12, 2022 ikionyesha chombo cha kubeba mizigo kwenye anga ya juu cha China, Tianzhou-5 kikiwa kimetekeleza minyumbuliko ya kiotomatiki na kutia nanga na muunganiko wa kituo cha anga ya juu cha China, Tiangong. (Picha na Sun Fengxiao/Xinhua)

BEIJING - Baada ya kukamilisha kazi zote zilizopangwa, chombo cha kubeba mizigo kwenye anga ya juu cha China, Tianzhou-5 kimetenganishwa na muunganiko wa kituo cha anga ya juu cha China, Tiangong majira ya saa 10:46 jioni (Saa za Beijing) na kubadilishwa kuwa chombo kinachojitegemea, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA).

Chombo hicho kitaingia tena kwenye mazingira ya angani chini ya udhibiti leo Jumanne. Sehemu zake nyingi zitachomwa moto na kuharibiwa wakati wa mchakato huo, wakati kiasi kidogo cha vifusi vitaanguka kwenye maji salama yaliyopangwa katika Bahari ya Pasifiki Kusini, CMSA imesema.

Chombo cha Tianzhou-5 kilirushwa kwenye obiti Novemba 12, 2022 kutoka Eneo la Urushaji Vyombo kwenye Angani ya juu la Wenchang katika mkoa wa kisiwa wa Hainan, Kusini mwa China.

Chombo hicho kilipeleka vifaa kwa wanaanga watatu waliosafiri kwenda anga ya juu kwa chombo cha Shenzhou-15 kwa ajili ya kukaa kwenye obiti kwa muda wa miezi sita. Pia kilipeleka vifaa vya kuzungusha chombo na vya majaribio, ikiwa ni pamoja na Satelaiti No.1 ya Sayansi ya Mwanafunzi wa Macao, seli za anga ya juu za mafuta ya hidrojeni-oksijeni, na chombo cha kugundua chembe zenye nishati nyingi.

Wakati wa safari yake kwenye obiti, kilijitenga na muunganiko wa kituo cha anga ya juu cha China Mei 5, kilitia nanga tena kwenye kituo hicho baada ya safari ya kujitegemea ya siku 33, na kuendelea kufanya majaribio ya teknolojia ya anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha