Rais Putin wa Russia asema nchi za Magharibi zinaharibu mfumo wa uhusiano wa kimataifa wa kifedha

(CRI Online) Septemba 13, 2023

Rais Vladimir Putin wa Russia akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wote wa Baraza la 8 la Uchumi la Mashariki (EEF) mjini Vladivostok, Russia, Septemba 12, 2023. (Picha na Guo Feizhou/Xinhua)

Rais Vladimir Putin wa Russia akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wote wa Baraza la 8 la Uchumi la Mashariki (EEF) mjini Vladivostok, Russia, Septemba 12, 2023. (Picha na Guo Feizhou/Xinhua)

VLADIVOSTOK - Uchumi wa Dunia unapitia mabadiliko kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kwamba baadhi ya nchi za Magharibi zinaharibu mfumo wa uhusiano wa kifedha, Rais Vladimir Putin wa Russia amesema Jumanne.

“Tunafahamu na kuona jinsi uchumi wa Dunia ulivyobadilika na unavyoendelea kubadilika katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ukweli kwamba baadhi ya nchi, hasa zile za Magharibi, zinaharibu mfumo wa uhusiano wa kifedha, kibiashara na kiuchumi ambayo wao wenyewe waliujenga.” Putin amesema katika hotuba yake aliyoitoa kwenye kikao cha wajumbe wote wa Baraza la 8 la Uchumi la Mashariki (EEF).

Amesema kuwa katika muktadha huu, ushirikiano wa kweli wa kibiashara kati ya mataifa ambayo yanachagua kutosalimu amri kwa shinikizo la nje unaongezeka. “Mataifa haya yanapendelea kufuata maslahi yao wenyewe,” Putin amebainisha.

Mji wa Mashariki ya Mbali wa Russia, Vladivostok ulikaribisha maelfu ya washiriki wa Baraza la 8 la Uchumi la Mashariki (EEF) siku ya Jumapili ili kuhimiza mabadilishano ya kiuchumi na kiutamaduni kati ya maeneo ya Asia-Pasifiki.

Baraza hilo litakalofanyika kwa siku nne limeandaliwa na Mfuko wa Roscongress. Likiwa na kauli mbiu ya "Kuelekea Njia ya Ushirikiano, Amani na Ustawi," Baraza hilo limetumika kama eneo muhimu la mazungumzo kati ya wanasiasa, wasimamizi wa biashara na wataalam kwa ajili ya maendeleo ya Mashariki ya Mbali na ushirikiano wa kikanda. 

Rais Vladimir Putin wa Russia (kati) akizungumza kwenye mkutano wa wajumbe wote wa Baraza la 8 la Uchumi la Mashariki (EEF) mjini Vladivostok, Russia, Septemba 12, 2023. (Xinhua/Cao Yang)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha