

Lugha Nyingine
Kiwango cha umaskini nchini Marekani chaongezeka Mwaka 2022 huku watoto wakiathirika zaidi
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Sensa ya Marekani, kiwango cha umaskini nchini humo kilipanda hadi asilimia 12.4 Mwaka 2022, huku umaskini wa watoto ukiongezeka maradufu kutoka Mwaka 2021.
Kipimo cha Kuongezeka Umaskini (SPM) ambacho kinapima iwapo watu wana rasilimali za kutosha kukidhi mahitaji yao kiliongezeka kwa asilimia 4.6 Mwaka 2022 kutoka mwaka wa nyuma yake. Takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa kiwango cha umaskini wa watoto kiliongezeka zaidi ya mara mbili, kutoka asilimia 5.2 Mwaka 2021 hadi asilimia 12.4 Mwaka 2022. Ni mabadiliko makubwa zaidi kwa umaskini wa watoto tangu ofisi hiyo ianze kufuatilia kipimo hicho Mwaka 2009.
Kwa mujibu wa Kituo cha Vipaumbele vya Bajeti na Sera, ambayo ni taasisi ya washauri bingwa wa mrengo wa kushoto ya Marekani, ongezeko la umaskini linamaanisha ongezeko la Wamarekani milioni 15.3 wanaoishi katika umaskini.
Rais wa Kituo cha Vipaumbele vya Bajeti na Sera Sharon Parrott amesema katika taarifa kwamba kupanda kwa kiwango cha umaskini kwa ujumla na kwa watoto, ambacho ni kikubwa zaidi katika rekodi ya zaidi ya miaka 50, kunasisitiza jukumu lililopo kwenye machaguo ya sera katika kiwango cha umaskini na ugumu wa maisha nchini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma