

Lugha Nyingine
Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini awasili Russia katika mji wa mpakani wa Khasan
Shirika Kuu la Habari la Korea (KCNA) limeripoti kuwa Kiongozi Mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amewasili Russia katika mji wa mpakani wa Khasan mapema Jumanne, ambapo yupo nchini humo kwenye ziara rasmi ili kuweka uhusiano wa urafiki na ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na Russia katika kiwango kipya cha juu.
Treni binafsi ya Kim iliingia kwenye Kituo cha Reli cha Khasan saa 12 asubuhi kwa saa za huko.
Kwenye mazungumzo yake na maafisa wa Russia katika chumba cha mapokezi cha kituo cha reli, Kim amesema kuwa ziara hiyo nchini Russia, ambayo ni ya kwanza ya nchi za nje tangu janga la COVID-19, ni uthibitisho wa wazi wa msimamo wa chama tawala na serikali ya Korea Kaskazini, kutoa kipaumbele kwa umuhimu wa kimkakati wa uhusiano kati ya pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma