Dunia inahitaji maridhiano, Katibu Mkuu UM Antonio Guterres asema

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kuelekea wiki ya ngazi ya juu ya Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Septemba 13, 2023. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku ya Jumatano kwamba ni kwa manufaa ya kila upande kuwa na maridhiano duniani.

Guterres ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kuelekea wiki ya ngazi ya juu ya Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kuanzia Septemba 18, viongozi na wajumbe kutoka nchi na mashirika mbalimbali duniani watakusanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani ili kushiriki katika mfululizo wa mikutano na shughuli za ngazi ya juu.

"Wito wangu kwa viongozi wa dunia utakuwa wazi," Guterres amesema. "Huu si wakati wa kutafuta ushawishi au kujiweka katika nafasi. Huu si wakati wa kutojali au kutofanya maamuzi. Huu ni wakati wa kukusanyika pamoja kwa ajili ya suluhu za kweli na za kivitendo. Ni wakati wa kupata maridhiano kwa ajili ya mustakabali mzuri."

"Siasa ni maridhiano. Diplomasia ni maridhiano. Uongozi bora ni maridhiano," ameongeza.

Amesema, viongozi wa dunia wanakusanyika wakati ambapo binadamu wanakabiliwa na changamoto kubwa, kutoka hali hatari za mabadiliko ya tabianchi iliyokuwa mbaya zaidi hadi migogoro yanayopamba moto, msukosuko wa gharama za maisha duniani, kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usawa na usumbufu mkubwa wa teknolojia.

"Watu wanawatazama viongozi wao kwa ajili ya utatuzi wa matatizo haya. Hata hivyo, katikati ya kukabiliana na haya yote na zaidi, mgawanyiko wa siasa za kijiografia unadhoofisha uwezo wetu wa kukabili hali," amesema.

Guterres ameeleza kuwa hali ya Dunia kuwa na ncha nyingi inaibuka. Ingawa nchi nyingi zenye nguvu inaweza kuwa sababu ya usawa wa nguvu duniani, inaweza pia kusababisha kuchochea mivutano, mgawanyiko na hali mbaya zaidi.

"Lakini wakati ambapo changamoto zetu zimeunganishwa zaidi kuliko hapo awali, matokeo ya mchezo wa kunufaisha upande mmoja ni kwamba kila mtu anapata hasara," amesema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (Nyuma) akipiga Kengele ya Amani kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, Septemba 13, 2023. (Cia Pak/Picha ya UN/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha