

Lugha Nyingine
Russia na Korea Kaskazini kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema na kuhimiza amani ya kikanda
Russia na Korea Kaskazini zitajitahidi kuimarisha uhusiano wa ujirani mwema na kuhimiza amani ya kikanda.
Hayo yamesemwa na Rais Vladimir Putin wa Russia alipokutana na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un siku ya Jumatano katika ukumbi wa Vostochny Cosmodrome, Mashariki mwa Russia.
Akikumbushia kwamba Umoja wa Kisovyeti ulikuwa wa kwanza kutambua mamlaka na uhuru wa Korea Kaskazini, Putin amesema wameazimia kuimarisha uhusiano wao wa urafiki na ujirani mwema, na kuongeza kuwa nchi zote mbili zitachukua hatua kwa jina la amani, utulivu na ustawi.
Kwa upande wake, Kim amebainisha kuwa ziara yake inafanyika wakati wa makabiliano makali katika nyanja za kimataifa, makabiliano kati ya maendeleo na mwitikio, haki na ukosefu wa haki, huku kukiwa na hali mpya ya Dunia yenye nchi nyingi zenye nguvu sawa.
Kim amesema amejadili hali ya kijeshi na kisiasa katika Peninsula ya Korea na Bara la Ulaya na mwenzake wa Russia, na kuongeza kuwa pande zote mbili zimekubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na kimbinu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma