China yasisitiza "mstari mwekundu wa kwanza" katika juhudi mpya za kutuliza uhusiano na Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2023

Picha iliyopigwa Septemba 17, 2021 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Picha iliyopigwa Septemba 17, 2021 ikionyesha jengo la Bunge la Marekani, Capitol huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)

Beijing - Kama sehemu ya juhudi zinazoendelea za kudumisha mawasiliano ya pande mbili na kuleta utulivu wa uhusiano, Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China na Mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Jake Sullivan, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani wamefanya mikutano ya duru nyingi huko Malta Jumamosi na Jumapili.

Kwenye mikutano hiyo, wamekubaliana kudumisha mabadilishano ya ngazi ya juu na kufanya mashauriano kuhusu mambo ya Asia-Pasifiki, mambo ya baharini pamoja na sera za mambo ya nje.

Hii ni mara ya pili kwa Wang kukutana na Sullivan katika muda wa miezi minne tangu mkutano wao mjini Vienna Mwezi Mei.

Pande hizo mbili zimefanya mawasiliano ya kimkakati kuhusu kuleta utulivu na kuboresha uhusiano kati ya China na Marekani.

"China inatumai kuwa uhusiano kati ya China na Marekani utarejea kwenye njia sahihi. Hili ni jambo la msingi," amesema Su Xiaohui, Naibu Mkurugenzi na mtafiti mshiriki wa Idara ya Masomo kuhusu Marekani katika Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Kimataifa ya China.

"Kwa mtazamo wa China, tunatumai kuwa uhusiano kati ya China na Marekani utaendelea kuwa tulivu," Su amesema. "China daima imekuwa ikisisitiza kwamba China na Marekani zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja ili kurudisha uhusiano kati ya pande mbili katika njia sahihi."

Wang Yi alipokutana na Sullivan amesisitiza kwamba suala la Taiwan ni mstari mwekundu wa kwanza ambao haupaswi kuvukwa katika uhusiano kati ya China na Marekani na upande wa Marekani lazima ufuate taarifa tatu za pamoja kati ya China na Marekani na kuheshimu ahadi yake ya kutounga mkono "Taiwan kujitenga na China."

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imefuata mkakati wa "ua mdogo, ukuta mrefu" kwa jina la kulinda usalama wa taifa. Licha ya kudai kuwa haina nia ya kutengana kiuchumi na China, Marekani imeendelea kuipiga China katika nyanja za teknolojia ya hali ya juu.

Wang amesema maendeleo ya China yana nguvu kubwa ya kujiendesha na yanafuata mantiki ya kihistoria ambayo haiwezi kuepukika na hayawezi kuzuiliwa. Haki halali ya watu wa China ya kupata maendeleo haiwezi kunyimwa, ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha