China yasema iko tayari kushirikiana na nchi wanachama wa G77 kuunda zama mpya ya maendeleo ya pamoja

(CRI Online) Septemba 19, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, Mkutano wa kilele wa Kundi la Nchi 77 (G77) na China uliofanyika hivi karibuni mjini Havana, Cuba, umetoa mchango chanya katika kuhamasisha nchi zinazoendelea ili kuimarisha umoja na ushirikiano na kukabiliana kwa pamoja na changamoto.

Amesema China iko tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Kundi hilo ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya Ulimwengu wa Kusini na kuunda zama mpya ya maendeleo ya pamoja.

Bibi Mao pia amesema kuwa, mkutano huo wa kilele umepitisha Azimio la Havana, linalosisitiza umoja na ushirikiano, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu kwa msingi wa mashauriano ya kina, ujenzi wa pamoja, na kunufaishana, kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu wote yenye mustakabali wa pamoja, na kunufaisha nchi na sehemu zote duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha