Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuwepo kwa mpango wa kimataifa wa kuokoa SDGs
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Malengo ya Maendeleo Endelevu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 18, 2023. (Xinhua/Li Rui)
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumatatu ametoa wito wa kuwepo kwa mpango wa kimataifa wa kuokoa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Nusu ya muda wa kutekeleza SDGs, ni asilimia 15 tu ya malengo ndiyo yamefikiwa na mengi yanarudi nyuma, Guterres amesema kwenye ufunguzi wa Mkutano wa SDG. "Badala ya kutomwacha mtu yeyote nyuma, tunakuwa na hatari ya kuacha nyuma SDGs."
“Kwa hiyo, malengo ya SDGs yanahitaji mpango wa kimataifa wa kuokoa,” amesema.
Ametoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kupunguza njaa, kuhamia kwa haraka kwenye nishati mbadala, kuenea zaidi kwa manufaa na fursa za maendeleo ya kidijitali, elimu bora kwa watoto na vijana, kutoa kazi zenye staha na ulinzi wa kijamii, na kuchukua hatua za mabadiliko ya tabianchi.
Miaka minane iliyopita, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilipitisha malengo ya SDGs, ambayo hayakuwa ahadi zilizotolewa na wanadiplomasia kwa kila mmoja bali ni ahadi kwa watu -- watu wanaoishi na umaskini, watu wanaokufa njaa katika Dunia yenye utajiri, watoto wanaokosa kiti darasani, familia zinazokimbia migogoro, wazazi wakitazama bila msaada watoto wao kufa na ugonjwa unaoweza kuzuilika, watu wanaopoteza matumaini kwa sababu hawawezi kupata kazi au ulinzi wa kijamii, jamii nzima inayokabiliana na maafa kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, amebainisha Guterres.
"Kwa hiyo, SDGs siyo malengo mfululizo. Yanabeba matumaini, ndoto, haki na matarajio ya watu ya kote duniani. Na yanatoa njia ya uhakika ya kuishi kwa mujibu wa majukumu yetu chini ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu, ambalo kwa sasa limetimiza mwaka wake wa 75," amesema.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Malengo ya Maendeleo Endelevu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 18, 2023. (Xinhua/Li Rui)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa Malengo ya Maendeleo Endelevu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Septemba 18, 2023. (Xinhua/Li Rui)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma