

Lugha Nyingine
Mapigano nchini Sudan yasababisha watu wengi zaidi kukimbia makazi yao
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulika na Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, mapigano mapya yanayoendelea katika Jimbo la Darfur Kusini nchini Sudan, haswa mjini Nyala, yamesababisha watu wengi zaidi kukimbia makazi yao.
OCHA imesema watu zaidi ya milioni 5.1 wamekimbia makazi yao tangu katikati ya Mwezi Aprili wakati mapigano nchini Sudan yalipotokea, na kati ya watu hao, zaidi ya milioni moja wamelazimika kutafuta hifadhi nje ya nchi.
Pia Ofisi hiyo imesema watoto wasiopungua 435 wameripotiwa kuuawa vitani na wengine 500 wamekufa kutokana na njaa, ingawa idadi halisi ni kubwa zaidi.
Ofisi hiyo imesema kuwa washirika wa kibinadamu wameongeza juhudi na wanaendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji makubwa licha ya uhaba wa fedha, huku watu milioni 3.5 wakipokea msaada tangu Mwezi Aprili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma