

Lugha Nyingine
IGAD yaboresha mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa katika maeneo ya mpakani nchini Kenya
Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limetoa vifaa tiba vyenye thamani ya dola za kimarekani milioni 8.95 kwa Kenya ili kuisaidia nchi hiyo kuwa na uwezo wa kufuatilia magonjwa katika maeneo ya mpakani.
Mkuu wa Tume ya IGAD nchini Kenya Fatuma Adan amesema, vifaa hivyo, ambavyo ni pamoja na kompyuta 7 za mkononi na kompyuta za mezani 37, vitatoa mchango mkubwa katika mradi wa Afya kwa Wote wa nchini humo. Amesema maendeleo ya kidijitali ni nguzo muhimu katika kuimarisha mifumo ya afya, ikiwemo mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa.
Ameongeza kuwa, nchi wanachama wa IGAD ziko katika mchakato wa kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kubadilishana taarifa na sera za ulinzi katika ngazi za kitaifa na kuvuka mpaka.
Katibu Mkuu wa Idara ya Afya ya Jamii na Vigezo vya Kitaalamu katika Wizara ya Afya nchini Kenya Mary Muriuki amesema, umuhimu wa vifaa hivyo unatokana na nafasi kubwa vitakavyochukua katika kuendeleza uratibu wa kuvuka mpaka na kuimarisha mwitikio wa changamoto mbalimbali zinazoathiri afya ya jamii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma