Wataalamu na wasomi wajadili mchango wa BRI kwa mambo ya haki za binadamu huko Geneva

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 20, 2023

Wataalamu na wasomi wa haki za binadamu wakishiriki kongamano lenye kaulimbiu ya "Ujenzi wa Pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na  Mambo ya Haki za Kibinadamu ya Dunia " huko Geneva, Uswisi, Septemba 19, 2023. (Xinhua/Lian Yi)

Wataalamu na wasomi wa haki za binadamu wakishiriki kongamano lenye kaulimbiu ya "Ujenzi wa Pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Mambo ya Haki za Kibinadamu ya Dunia" huko Geneva, Uswisi, Septemba 19, 2023. (Xinhua/Lian Yi)

GENEVA - Kongamano linaloangazia maendeleo ya mambo ya haki za binadamu katika nchi zinazoshiriki katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) limefanyika siku ya Jumanne mjini Geneva, Uswisi.

Katika kongamano hilo, wataalam na wasomi wa haki za binadamu kutoka China na nchi nyingine wamebadilishana maoni yao kuhusu mchango wa ushirikiano wa BRI katika maendeleo ya kimataifa na mambo ya haki za binadamu.

Kongamano hilo lenye kaulimbiu ya "Ujenzi wa Pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Mambo ya Haki za Binadamu ya Dunia" limeandaliwa na Mfuko wa China wa Maendeleo ya Haki za Binadamu, ambao ni shirika lisilo la kiserikali la China linalojishughulisha na kuhimiza mambo ya haki za binadamu.

Naibu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa shirika hilo Zuo Feng amesema tangu pendekezo hilo lililotolewa na China Mwaka 2013, zaidi ya nchi 150 na mashirika 30 ya kimataifa yamesaini makubaliano ya ushirikiano.

Amesema, katika muongo mmoja uliopita, ushirikiano wa BRI umekuwa na jukumu la kiujenzi katika kuboresha hali ya uchumi wa kimataifa, kukuza maendeleo na ustawi wa pamoja, na kuboresha mfumo wa usimamizi wa kimataifa.

“Inatambulika kwa upana kuwa ushirikiano wa BRI umetoa mchango chanya katika maendeleo ya kimataifa na mambo ya haki za binadamu” amesema.

Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya mikutano kuhusu mambo ya haki za binadamu ya dunia kwenye Mkutano wa 54 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaoendelea kuanzia Septemba 11 hadi Oktoba 13. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha