

Lugha Nyingine
China yaipita Marekani katika kuchapisha tasnifu za kitaaluma zenye ushawishi mkubwa: ripoti
Timu ya utafiti ya kimataifa inayoongozwa na wataalamu wa unajimu wa China imefichua vipengele vyenye utatanishi vinavyobadilika vya jeti za shimo jeusi, kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Nature. (Xinhua/Ou Dongqu)
BEIJING - China imechangia karibu theluthi moja ya tasnifu za kitaaluma zilizochapishwa kwenye majarida ya kimataifa yenye ushawishi mkubwa zaidi Mwaka 2022, ikiwa ni mara ya kwanza China kuipiku Marekani na kupata nafasi ya juu duniani, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatano.
Miongoni mwa tasnifu za kitaaluma zaidi ya 54,002 zilizochapishwa mwaka jana kwenye majarida 159 yenye ushawishi mkubwa zaidi wa mchango katika taaluma 178, tasnifu zaidi ya 16,349 zilichangiwa na waandishi wa China, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Upashanaji Habari za Sayansi na Teknolojia ya China (ISTIC) chini ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China.
Katika tasnifu za kitaaluma karibu 350,000 za kiwango cha juu zilizochapishwa katika majarida 371 ya kimataifa yenye ushawishi mkubwa na manukuu mengi, takriban asilimia 27 ya tasnifu hizi zimeshuhudia waandishi wake wa kwanza wakitoka katika taasisi za China. Tasnifu hizo za kitaaluma zimenukuliwa takriban kwa mara 650,000, huku China ikishika nafasi ya kwanza duniani katika idadi ya tasnifu za kitaaluma zilizochapishwa na idadi ya manukuu.
Mwaka 2022, China ilichukua nafasi ya pili kwa kuchapishwa kwa tasnifu za kitaaluma na makala za maelezo zilizochapishwa katika majarida 16 ya juu ambazo zilijivunia ushawishi wa mchango wa kitaaluma zaidi ya 30 na zimenukuliwa kwa mara zaidi ya 100,000, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Kwa kuendana na Fahirisi ya Jarida la Nature Mwaka 2023 lililochapishwa Mwezi Juni ambalo lilifichua kuwa Mwaka 2022, China iliipita Marekani kwa uwiano wa tasnifu za kitaaluma zilizochapishwa kwenye majarida yenye ushawishi wa juu katika uwanja wa sayansi ya mazingira asilia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma