Mjumbe wa China azungumzia haki za wanawake wenye ulemavu katika mkutano wa baraza la haki za binadamu la UN

(CRI Online) Septemba 22, 2023

Mjumbe wa Kudumu wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva na mashirika mengine ya kimataifa nchini Uswisi Balozi Chen Xu, ametoa hotuba siku ya Alhamisi kwa niaba ya nchi zaidi ya 80 kuhusu masuala ya kulinda haki za wanawake wenye ulemavu kwenye mkutano wa 54 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Kwenye hotuba yake hiyo, Balozi Chen amesema japo sasa mambo yanayohusu wanawake yamepata maendeleo makubwa duniani, lakini wanawake wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uhakikisho wa kijamii, ubaguzi na umaskini huku akisisitiza kuwa kuhimiza maendeleo jumuishi ya jamii ni njia muhimu ya kuwanufaisha wanawake hao, ambayo itachangia kuhimiza usawa katika maisha na maendeleo yao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha