Waziri Mkuu wa China Li Qiang akutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2023

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Septemba 25, 2023. Rais wa Syria aliwasili China  kushiriki kwenye sherehe za  kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia iliyofanyika Hangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Xinhua/Rao Aimin)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Septemba 25, 2023. Rais wa Syria aliwasili China kushiriki kwenye sherehe za kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia iliyofanyika Hangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Xinhua/Rao Aimin)

BEIJING- Waziri Mkuu wa China Li Qiang amekutana na Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Beijing siku ya Jumatatu ambaye aliwasili China kushiriki kwenye sherehe za kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia iliyofanyika Hangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China ambapo amesema kuwa urafiki kati ya China na Syria umekuwa na historia ndefu, na nchi hizo mbili ni marafiki wa kweli wanaosimama pamoja katika hali ngumu na nzuri.

“Viongozi wakuu wa nchi mbili kwa pamoja wametangaza kuanzishwa kwa uhusiano wa kimkakati kati ya China na Syria huko Hangzhou, na kuweka muongozo mpya wa maendeleo ya uhusiano wa pande hizo mbili” Waziri Mkuu Li amesema.

Ameeleza kuwa China iko tayari kujiunga na Syria katika kutekeleza maoni muhimu ya pamoja ya viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, kusukuma mbele mafanikio mapya katika ushirikiano wa pande mbili na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Amesema China itaendelea kuiunga mkono Syria kithabiti katika kulinda uhuru wake, mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali ya nchi yake, na kupinga kithabiti uingiliaji wa nje katika masuala ya ndani ya Syria.

Waziri Mkuu Li ameongeza kuwa China inakaribisha ushiriki wa Syria katika Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, itaendelea kuunga mkono ukarabati, urejeaji katika hali ya kawaida na maendeleo ya Syria, na iko tayari kupanua mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara ya pande mbili na Syria, na kuhimiza maelewano na ushirikiano kati ya watu wa pande hizo mbili.

Kwa upande wake Rais Assad ameeleza shukrani zake kwa msaada wa China katika kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Syria, kupunguza janga la ubinadamu na kutoa msaada wakati nchi hiyo ilipokumbwa na tetemeko la ardhi.

“China inatoa mchango muhimu katika masuala ya kimataifa” Amesema Rais Assad na kuongeza kuwa Syria itashirikiana na China katika kutekeleza Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha