Lugha Nyingine
China yatoa waraka kuhusu Kufanya Kazi Pamoja Kujenga Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja wa Binadamu
Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka unaoitwa “Kufanya Kazi Pamoja Kujenga Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja wa Binadamu: Mapendekezo na Hatua za China.”
Kwa mujibu wa waraka huo, miaka kumi iliyopita, Rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, ambalo lilitoa nuru wakati dunia ilipokuwa ikikabiliwa na hali ya sintofahamu, na kuwakilisha mchango wa China katika juhudi za kimataifa za kulinda dunia ya pamoja na kujenga siku bora za baadaye zenye ustawi kwa watu wote.
Waraka huo umesema, ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, binadamu wote, nchi zote, na kila mtu ni lazima kusimama pamoja katika shida na raha, na kusonga mbele kwa mapatano zaidi katika dunia ambayo kila mmoja anaiita nyumbani kwake.
Waraka huo umetoa wito kwa juhudi zaidi katika kujenga dunia wazi, jumuishi, safi na nzuri ambayo inafurahia amani ya kudumu, usalama kwa wote, na ustawi wa pamoja, na kubadili matarajio ya muda mrefu ya watu kuwa na maisha bora kuwa uhalisia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



