Barabara ya Kenya iliyojengwa na China yatunukiwa tuzo ya kikanda

(CRI Online) Septemba 26, 2023

Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi iliyojengwa na China nchini Kenya imepewa tuzo ya “uvumbuzi bora wa teknolojia katika sekta ya usafiri” kwenye awamu ya pili ya Tuzo za Afrika Mashariki.

Kampuni iliyojenga na kuendesha barabara hiyo imepewa tuzo hiyo kutokana na mfumo wake wa kielektroniki wa kutoza ada ya matumizi ya barabara (ETC), ambao ni uvumbuzi unaoruhusu waendesha magari kulipa moja kwa moja kutoka kwenye kadi za kielektroniki zilizofungwa kwenye magari wanapotumia barabara hiyo.

Ili kuwezesha huduma hiyo, mtu hujiandikisha kwa kutoa nakala ya kitambulisho na kitabu chake cha kumbukumbu, na gari lake huwekwa kadi hiyo yenye chip ambayo itawawezesha watu kulipia huduma hiyo kwa kuingiza pesa. Mfumo wa ETC unavutia waendesha magari kwani unaokoa muda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha