Rais Xi Jinping asisitiza ujenzi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria ya kiwango cha juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2023

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesisitiza kufanya juhudi za kujenga maeneo ya majaribio ya biashara huria ya kiwango cha juu (FTZs), na kuyataka maeneo hayo yaliyoanzishwa yatangulie mbele katika kutafuta maendeleo mapya na kukabiliana na changamoto ngumu.

Rais Xi amesisitiza hayo kwenye maagizo yake ya hivi karibuni ya kuendeleza ujenzi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria.

“Ujenzi wa maeneo ya biashara huria umekuwa hatua muhimu ya kimkakati ya Kamati Kuu ya CPC kuendeleza mageuzi na ufunguaji mlango katika zama mpya,” amesema.

Ameeleza kuwa, katika muongo mmoja uliopita, maeneo ya biashara huria yametumika kama majukwaa ya majaribio ya sekta zote kwa ajili ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa kuchochea idadi kubwa ya sera za kimsingi na za kupigiwa mfano na kufikia matokeo mengi ya kihistoria na uongozi katika uvumbuzi.

Amesisitiza kuwekwa mikakati ya kuboresha maeneo ya biashara huria katika safari mpya ya China, kwa kufanya majumuisho kuhusu uzoefu wa muongo mmoja uliopita, akisema maeneo hayo yanapaswa kutangulia mbele katika kutafuta maendeleo mapya kwenye nyanja mpya, kukabiliana na changamoto ngumu na kufanya uchunguzi mpana na wa kina.

Amesema maeneo ya biashara huria yanaweza kutekeleza majukumu ya kupigiwa mfano zaidi katika ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, kujikita katika uvumbuzi, kuratibu maendeleo na usalama, kuendana na kanuni za uchumi na biashara za kimataifa, ili kutimiza utekelezaji wa mkakati wa kufungua mlango kwa uvumbuzi wa utaratibu, na kusukuma mbele maendeleo ya kutegemea uvumbuzi kwenye mnyororo wa viwanda.

Maagizo hayo ya Rais Xi yamewasilishwa na Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng kwenye mkutano uliofanyika Beijing siku ya Jumanne kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa eneo la biashara huria la kwanza nchini China.

Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa maagizo ya Rais Xi Jinping kuhusu kuendeleza ujenzi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria (FTZs) na kutoa hotuba kwenye mkutano wa Beijing wa kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa eneo la biashara huria la kwanza nchini China, Septemba 26, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa maagizo ya Rais Xi Jinping kuhusu kuendeleza ujenzi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria (FTZs) na kutoa hotuba kwenye mkutano wa Beijing wa kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa eneo la biashara huria la kwanza nchini China, Septemba 26, 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha