Kusukuma kikomo: Safari ya kukimbia ya msichana wa miaka 16 nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 02, 2023

Akifuata kauli mbiu yake "Uwezo wa binadamu hauna kikomo, na ninataka kujua kikomo changu kiko wapi," Msichana Zhen Xin wa China mwenye umri wa miaka 16 tayari ameshinda changamoto nyingi ambazo zinaweza kuwashangaza hata watu wazima.

Msimu huu wa majira ya joto, Zhen alikamilisha kazi ya ajabu ya kupanda milima mitano mikubwa ya China. Katika muda wa siku nne na saa kumi tu, alifanikiwa kuuteka Mlima Huashan, Mlima Songshan, Mlima Taishan, Mlima Hengshan katika Mkoa wa Shanxi, Kaskazini mwa China, na Mlima Hengshan ulioko Mkoa wa Hunan, Katikati mwa China. Kwa kufanya hivyo, amekuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi na mwenye kutumia kasi zaidi kukamilisha changamoto hiyo.

Siyo mara ya kwanza kwa Zhen kukabiliana na changamoto kama hizo -- kuanzia na mbio zake za marathon za kwanza akiwa na umri wa miaka 11, sasa amekamilisha marathoni 13. Atakapofikia umri wa miaka 18, anataka kushiriki Shindano la Dunia la Mbio za Marathon, ambalo linahusisha kukimbia mbio saba za marathoni katika mabara saba ndani ya siku saba.

Huku akiwa bado katika shule ya sekondari, msichana huyu kijana mwenye kudhamiria, ambaye mara kwa mara anasukuma vikomo vya uwezo wake mwenyewe, ana mipango ya kusoma shahada ya kwanza ya saikolojia katika chuo kikuu, "kwa sababu ninataka kugundua visivyojulikana," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha