Safari zaidi ya milioni 100 zafanywa kwenye reli za China katika wiki moja huku kukiwa na ongezeko la safari za likizo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 05, 2023

Abiria wakisubiri treni kwenye ukumbi wa abiria kusubiri kupanda treni wa Stesheni ya Reli ya Chongqing Kaskazini huko Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Septemba 29, 2023. (Xinhua/Liu Chan)

Abiria wakisubiri treni kwenye ukumbi wa abiria kusubiri kupanda treni wa Stesheni ya Reli ya Chongqing Kaskazini huko Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Septemba 29, 2023. (Xinhua/Liu Chan)

BEIJING – Reli za China zimerekodi safari za abiria zaidi ya milioni 17 siku ya Jumanne, na kufanya jumla ya safari zilizofanywa kwenye reli kufikia milioni 114 katika siku saba zilizopita, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Jumatano na Kundi la Kampuni za Shirika la Reli la China, ambalo ni mwendeshaji wa reli nchini China.

Katika taarifa yake, shirika hilo limesema kuwa shughuli za reli zimekuwa salama, tulivu, na zenye kuendeshwa kwa utaratibu tangu Septemba 27 siku ya kuanza kwa pilika pilika za usafiri kwa ajili ya siku nane za likizo ya Siku ya Kijadi ya Mbalamwezi na Siku ya Taifa la China, ambayo ilianza rasmi Septemba 29 hadi Okt. 6 mwaka huu.

Shirika hilo limekadiria kuwa safari za abiria za reli zitaendelea kuwa katika kiwango cha juu na kufikia milioni 17.3 siku ya Jumatano, wakati treni 11,679 zitatumika kukidhi mahitaji ya usafiri.

Limeongeza kuwa kilele kingine cha pilika za watu wengi kusafiri kitaonekana Oktoba 5 na Oktoba 6 watalii wanaporejea nyumbani baada ya likizo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha