Kevin McCarthy aondolewa kwenye nafasi ya Spika wa Bunge la Marekani kutokana na mgongano wa wabunge wa Chama cha Republican

(CRI Online) Oktoba 05, 2023

Baraza la Wawakilishi la Marekani linalodhibitiwa na chama cha Republican limepitisha hoja ya kumuondoa madarakani Spika Kevin McCarthy siku ya Jumanne katika hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa kutokana na mgongano wa wabunge wa chama cha Republican, baada ya McCarthy kuegemea kura za chama cha Democratic kupitisha mswada wa bajeti "safi" wa kuondoa tatizo kwa muda ili kuepusha kufungwa kwa shughuli za serikali kuu ya Marekani.

Baraza hilo, linalozidi kidogo tu wingi wa kura za Republican, limepitisha hoja hiyo kwa kura 216-210, huku wabunge wa Chama cha Republican wanane wakiungana na wale wa Chama cha Democrat kumwondoa McCarthy katika nafasi yake.

Kura hiyo ilikuja chini ya siku moja baada ya Mbunge mwenye msimamo mkali wa Chama cha Republican Matt Gaetz kutangaza azimio la kumuondoa McCarthy kupitia mchakato unaojulikana kama ‘hoja ya kuondoka’.

Gaetz na Wabunge wengine wa Chama cha Republican wenye misimamo mikali wamekuwa wakionya kwa wiki kadhaa kwamba wangechukua hatua ya kumwondoa McCarthy kwenye wadhifa wake wa kuwa kiongozi wa bunge ikiwa ataegemea upande wa wabunge wa Chama cha Democrat kupitisha sheria ya bajeti.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha