Fikra ya Xi Jinping juu ya Utamaduni yatolewa kwa umma kwenye mkutano wa taifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2023

BEIJING – Fikra ya Xi Jinping juu ya Utamaduni imetolewa rasmi kwa umma kwenye mkutano wa taifa wa siku mbili nchini China kuhusu kazi za uenezi, fikra na utamaduni, ambao umefanyika Beijing Jumamosi na Jumapili.

Tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mafanikio ya kihistoria yamepatikana katika nyanja za uenezi wa kiumma na utamaduni, mkutano huo umeeleza kuwa, mafanikio hayo yanatokana na uongozi wa Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC).

Mawazo mapya na kipimo kipya kuhusu maendeleo ya kitamaduni katika zama mpya yaliyotolewa na Rais Xi yameboresha na kuendeleza nadharia ya utamaduni ya Umarx na kuleta Fikra ya Xi Jinping juu ya Utamaduni, mkutano huo umeeleza.

Maagizo ya hivi karibuni ya Rais Xi yaliwasilishwa kwenye mkutano huo.

Katika maagizo hayo, Rais Xi amesisitiza kujenga kujiamini kithabiti katika utamaduni, kufuata mbinu ya uwazi na ujumuishaji, na kushikilia kanuni za msingi huku maendeleo mapya yakitafutwa ili kutoa hakikisho thabiti la kiitikadi, nguvu ya kiroho na hali nzuri ya kitamaduni kwa ajili ya kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika mambo yote na kuendeleza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China kwa pande zote.

Katika maagizo yake Rais Xi ameeleza kuwa kazi ya uenezi wa kiumma na utamaduni ni muhimu sana, tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, Kamati Kuu ya CPC imefanya mipango na mipangilio ya kimfumo katika suala hili kutoka kwenye mtazamo wa jumla na wa kimkakati, ili kupata mafanikio ya kihistoria katika lengo hili.

Mkutano huo umedhihirisha kuwa, Fikra ya Xi Jinping juu ya Utamaduni ni mfumo wa fikra unaoendelezwa na ni uwazi,ambao utaboreshwa na kuendelezwa kadiri utekelezaji wake kwa vitendo unavyoendelea, mkutano huo pia umehimiza kufanya juhudi zaidi katika kusoma, kutafiti na kutafsiri fikra hiyo.

Cai Qi, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni  katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu ya CPC, akihudhuria na kutoa hotuba kwenye mkutano kuhusu kazi ya uenezi, fikra na utamaduni ya nchi nzima  uliofanyika Beijing, China. (Xinhua/Yao Dawei)

Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Ofisi ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, akitangaza mpango kazi kwenye mkutano kuhusu kazi ya uenezi, fikra na utamaduni ya nchi nzima uliofanyika Beijing, China. (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha