

Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa Palestina na Israeli kusitisha mara moja mapigano
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema China inafuatilia hali ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Palestina na Israeli, na kutoa wito kwa pande zote zinazohusika kudumisha utulivu na kujizuia kuchochea hali, kusitisha mara moja mapigano ili kulinda raia na kuzuia kuzorota zaidi kwa hali hiyo.
Msemaji wa wizara hiyo ameyasema hayo wakati akijibu swali kuhusu mapigano makali yanayoendelea kati ya Israeli na makundi yenye silaha katika Ukanda wa Gaza wa Palestina ambayo yamesababisha idadi kubwa ya vifo kutoka pande zote mbili.
Pia imesema mapigano hayo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara yameonesha kuwa kukwama kwa muda mrefu kwa mchakato wa amani hakupaswi kudumishwa.
Wizara hiyo imesema, njia ya kutuliza mgogoro huo ni kutekeleza “Suluhu ya Nchi Mbili”, na kuunda nchi huru ya Palestina.
Imesema, Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza ufuatiliaji katika suala la Palestina, kuhimiza kurejeshwa mapema kwa mazungumzo kati ya Palestina na Israeli, na kutafuta njia ya kudumu ya amani. Pia imesisitiza kuwa China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi bila ya kusita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma