

Lugha Nyingine
China yatoa salamu za rambirambi kuomboleza vifo vya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan
(CRI Online) Oktoba 09, 2023
China imetoa salamu za dhati za kuomboleza vifo vya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea katika Jimbo la Herat, Afghanistan, na kutoa rambirambi kwa familia za waathirika.
Salamu hizo zimetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya China wakati msemaji wake akijibu maswali kuhusu tetemeko hilo lililotokea nchini Afghanistan.
Wizara hiyo pia imesema inaamini kuwa watu wa Afghanistan wataweza kushinda athari zinazoletwa na janga hilo na kujenga upya mapema nchi yao, na kwamba China itatoa msaada kadiri iwezavyo kutokana na mahitaji ya Afghanistan.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma