Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi nchini Afghanistan yafikia 2,445

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2023

Picha iliyopigwa tarehe 8, Oktoba, 2023 ikionesha vifusi vya makazi ya Waafghanistan

Picha iliyopigwa tarehe 8, Oktoba, 2023 ikionesha vifusi vya makazi baada ya tetemeko la ardhi lililotokea huko Herat, Afghanistan. (Picha ilipigwa na Saifurahman Safi/Xinhua)

Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi huko Herat, Magharibi mwa Afghanistan na majimbo jirani imeongezeka hadi 2,445, amesema Mawlawi Musa Ashari, kiongozi wa Idara ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Afghanistan katika Jimbo la Herat usiku wa Jumapili.

Eneo lililoathiriwa vibaya zaidi ni Wilaya ya Zanda Jan katika jimbo hilo la Herat, ambako vijiji 13 “vimebomolewa kabisa”, amesema Ashari.

Mapema ya siku hiyo, Msemaji wa Idara ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa ya Afghanistan, Mullah Janan Shaeq alisema, watu zaidi ya 9,200 wamejeruhiwa katika matetemeko ya ardhi.

Kwa mujibu wa Kituo cha Mtandao wa Tetemeko la Ardhi cha China, matetemeko mawili ya ardhi yenye ukubwa wa 6.2 katika kipimo cha Richter yalitokea nchini Afghanistan siku ya Jumamosi. Tetemeko la kwanza lilitokea saa 5:10 hivi kwa saa za Herat.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha