Liberia yasema iko tayari kuimarisha uhusiano na China ili kutimiza maendeleo ya pamoja

(CRI Online) Oktoba 11, 2023

Serikali ya Liberia imesema iko tayari kuimarisha uhusiano na China, na kukuza ushirikiano wa kunufaishana ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

Rais wa Liberia George Weah amesema hayo alipopokea hati za utambulisho za Balozi mpya wa China nchini humo Yin Chengwu. Rais Weah amesisitiza kuwa Liberia inafuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na kuishukuru China kwa msaada wake wa kusaidia maendeleo ya nchi hiyo na kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake Balozi Yin Chengwu amesema, China inatilia maanani sana kuendeleza uhusiano na Liberia, na iko tayari kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili kwa kufuata msingi wa kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na kunufaishana. Pia iko tayari kuongeza kuaminiana kisiasa, na kuhimiza ushirikiano wa kiwenzi wa pande zote kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo mapya.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha