

Lugha Nyingine
Baraza la Mawaziri la wakati wa vita la Israeli laapa "kuiangamiza" Hamas, huku AL ikitoa wito wa kusitisha mapigano mara moja
Washiriki wakihudhuria mkutano maalum wa mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) kwenye makao makuu ya AL huko Cairo, Misri, Oktoba 11, 2023. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
JERUSALEM - Baraza jipya la mawaziri la Israel maalum kwa ajili ya wakati wa vita limeapa siku ya Jumatano kuendelea na operesheni ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza hadi pale "Kundi la Hamas litakapopinduliwa na kuangamizwa" huku Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) ikitoa wito wa kusitisha mara moja mapigano yanayoendelea na kurejesha mchakato wa amani uliokwama.
Kauli hiyo ya baraza jipya la mawaziri la Israel maalum kwa ajili ya wakati wa vita ni ya kwanza tangu kuundwa kwa serikali mpya ya dharura ya umoja wa kitaifa mapema Jumatano huku Benny Gantz, kiongozi wa upinzani na waziri wa zamani wa ulinzi wa Israeli, akijiunga na serikali ya mseto ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yenye mrengo uliopitiliza wa kitaifa na kidini.
Katika hotuba kwa taifa iliyorushwa na vyombo vya habari, Gantz ameapa kushughulika "kikamilifu" na kundi la Hamas.
"Tutaiangamiza na kuharibu Hamas," Netanyahu amesema.
Wakati huohuo mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) wametoa wito siku ya Jumatano wa kusitisha mara moja mapigano yanayoendelea kati ya Israel na Gaza na kurejesha mchakato wa amani uliokwama kati ya Palestina na Israel.
Katika taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano maalum wa mawaziri wa mambo ya nje wa AL uliofanyika Cairo, wanadiplomasia hao waandamizi wamezitaka pande zote kujizuia na kuonya juu ya "athari mbaya za kibinadamu na usalama" baada ya mgogoro huo kupamba moto zaidi.
Wamesisitiza umuhimu wa Israel kuondoa udhibiti kamili kwenye Ukanda wa Gaza na kutoa mara moja misaada ya kibinadamu, chakula na mafuta kwa wakazi wa Gaza.
Hamas siku ya Jumamosi lilianzisha mashambulizi ya kushtukiza katika miji ya Israel inayopakana na Ukanda wa Gaza, na kuifanya Israel ifanyae mashambulizi ya kulipiza kisasi Gaza.
Hadi kufikia Jumatano, watu zaidi ya 2,000 wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa kwa pande zote mbili.
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2023 ikionyesha mwanajeshi akiwa kwenye jengo lililobomolewa katika mashambulizi ya roketi kutoka Gaza, huko Ashkelon, Israel. (Ilan Assayag/JINI kupitia Xinhua)
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2023 ikionyesha ukuta uliobomolewa katika mashambulizi ya roketi kutoka Gaza, huko Ashkelon, Israel. (Ilan Assayag/JINI kupitia Xinhua)
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2023 ikionyesha wanajeshi na gari la zimamoto likiwa mbele ya jengo lililobomolewa katika mashambulizi ya roketi kutoka Gaza, huko Ashkelon, Israel. (Ilan Assayag/JINI kupitia Xinhua)
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2023 ikionyesha jengo lililobomolewa katika mashambulizi ya roketi kutoka Gaza, huko Ashkelon, Israel. (Ilan Assayag/JINI kupitia Xinhua)
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2023 ikionyesha ukuta uliobomolewa katika mashambulizi ya roketi kutoka Gaza, huko Ashkelon, Israel. (Ilan Assayag/JINI kupitia Xinhua)
Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2023 ikionyesha mtu akitembea kuupita ukuta uliobomolewa katika mashambulizi ya roketi kutoka Gaza, huko Ashkelon, Israel. (Ilan Assayag/JINI kupitia Xinhua)
Watu wakikagua majengo yaliyobomolewa kwenye mashambulizi ya anga ya Israel katika mji wa Kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah, Oktoba 11, 2023. (Khaled Omar/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma