

Lugha Nyingine
Ziara ya kutia moyo iliyofanyika China: Mwalimu wa Malta asifu Kujenga kwa PamojaUkanda Mmoja, Njia Moja
Martin Azzorpardi, mwanzilishi wa "Kona ya China" na mwalimu wa sayansi katika Shule ya Sekondari ya Chuo cha St. Margaret huko Malta, hivi karibuni amepongeza Kujenga kwa Pamoja Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lililopendekezwa na China katika mahojiano maalum na People's Daily Online.
Azzorpardi ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya China kwa kuanzisha jukwaa ambalo linahimiza mazungumzo ya kitamaduni na ushirikiano kati ya nchi mbalimbali.
"Nina furaha kusema kwamba Malta ilikuwa moja ya nchi za kwanza kujiunga na BRI. Hiki ndicho tunachohitaji siku hizi," Azzorpardi amesema. "Hatutaki vita. Tunahitaji kushikamana. Tunahitaji kunufaika pamoja utamaduni wa kila mmoja wetu na pia kubadilishana mawazo yetu na kujifunza jinsi ya kufanya kazi pamoja."
Kuvutiwa kwa Azzorpardi na utamaduni wa China kulichochewa wakati wa ziara yake kuhusu mageuzi nchini China Mwaka 2010. Alisafiri katika miji yenye shughuli nyingi kama vile Shanghai, Beijing, na Hong Kong, tajriba ambayo ilimgusa sana.
Baada ya kurudi Malta, alijitolea kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni kati ya Malta na China.
Mwaka 2020, Azzorpardi na wenzake na wanafunzi kutoka "Kona ya China" walimwandikia barua Rais Xi Jinping. Walionyesha kupendezwa kwao na utamaduni wa China na kusifu maono ya mustakabali wa pamoja wa binadamu, kama ulivyowakilishwa na BRI.
Akiwa pamoja na mmoja wa wanafunzi wake na marafiki kadhaa wa kimataifa, hivi karibuni Azzorpardi amepata fursa ya kutembelea maeneo mengi nchini China, ikiwa ni pamoja na Liangjiahe, kijiji kidogo cha Yan'an kilichoko Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, ambako Rais Xi Jinping wa China alitumia sehemu ya miaka yake ya malezi.
Ziara hizi zimeongeza uelewa wa Azzorpardi kuhusu maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya China katika miongo kadhaa iliyopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma