

Lugha Nyingine
Safari ya Kuongeza Mabadilishano na Maelewano kati ya China na Nchi za Nje: Mazungumuzo ya Kirafiki kando ya Mto Huangpu, Mjini Shanghai
Ujumbe wa wageni kutoka nchi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja kwenye Kituo cha Makazi cha Gubei. (Picha ilipigwa na Zhang Rong/People's Daily Online)
Asubuhi ya tarehe 11, ujumbe wa wageni kutoka nchi mbalimbali ulioalikwa na Mfuko wa Maendeleo na Amani wa China uliwasili Shanghai, China. Ujumbe huo umepata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali kando ya Mto Huangpu kuanzia Kituo cha Makazi cha Gubei, Jumba la Makumbusho ya Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mpaka Jumba la Maonyesho la Mipango Miji na Jengo la Televisheni ya “Lulu ya Mashariki (Oriental Pearl)”, wakihisi kwa kina hali ya kuwepo kwa mapatano ya mandhari ya historia na utamaduni na ustawi na maendeleo ya kijamii ya mji huo.
Kuingia kwenye jumuiya za makazi na kujionea uhalisia wa maisha na furaha ya wakazi
Kwanza ujumbe huo ulikwenda kwenye Kituo cha Makazi cha Gubei kilichoko katika Mtaa wa Hongqiao wa Eneo la Changning la Mji wa Shanghai, ambapo kuna “bustani ya watoto”, “kituo cha huduma ya chakula kwa wazee” na vituo vya huduma nyingine mbalimbali.
Seti ya chakula chenye thamani ya bei Yuan 18 (takriban Dola za Kimarekani 2.5) inayokamilishwa na mboga za majani na nyama kwenye kituo hicho cha huduma ya chakula kwa wazee ilivutia macho ya Amangeldiyev Sapargeldi, mwanafunzi kutoka Turkmenistan anayesomea shahada ya uzamivu (PhD) katikaChuo Kikuu cha Peking. “Kwakweli bei ni nafuu sana,” alisema huku akiangalia ubao wa menyu mlangoni, “Kituo hiki (Makazi cha Gubei) kinaleta urahisi sana. Hivi sasa vijana huenda kazini kwa hivyo hawana muda wa kuwahudumia wazee na watoto. Hapa usalama na elimu vimehakikishwa.”
Kutazama historia ya nyuma na kuelewa “mwanzo hodari” wa CPC
“Ikiwa ni sehemu ya kuzaliwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China, eneo la Jumba la Mkutano Mkuu wa Kwanza wa CPC linabeba juhudi na kujitoa mhanga kwa mashujaa wa mapinduzi ya China. Kutembelea jumba hilo kunawawezesha wageni waelewe zaidi historia ya mapinduzi ya China,” amesema mjumbe Zoon Ahmed baada ya kutembelea jumba hilo, “mashujaa wa mapinduzi ya China walijitoa mhanga kwa mengi na kufanya jududi nyingi, na moyo huu ambao hurithishwa kizazi hadi kizazi.”
Maadhimisho ya Kutimia Miaka 10 ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" yamewezeshwa kwa muunganisho wa kiroho
Mwaka huu inatimia miaka 10 tangu kutolewa kwa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Katika mwongo uliopita, chini ya juhudi za pande zote husika, ujenzi wa pamoja wa pendekezo hilo umebadilishwa hatua kwa hatua kutoka kuwa wazo hadi vitendo, na kutoka maono hadi uhalisia.
Israt Amin, mwongozi wa televisheni ya Channel 24 ya Bangladesh akiwa amesimama kando ya Mto Huangpu alisema kuwa, “Pendekezo la ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’ limehimiza ujenzi wa miundombinu katika sekta ya usafiri, nishati na mawasiliano na nyinginezo, na pia kukuza mabadilishano ya kitamaduni.” Aliongeza kuwa, ujenzi wa pendekezo hilo umetoa uungaji mkono wa kiroho kwa muunganisho na maelewano kati ya watu.
Israt Amin akihojiwa kwenye eneo la Huangpubinjiang mjini Shanghai. (Picha ilipigwa na Zhang Rong/People's Daily Online)
Geoffrey Loi kutoa Papua New Guinea ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya mpira wa mezani ya nchi hiyo ameshukuru pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, “Kwa kupitia pendekezo hilo muhimu, Papua New Guinea na China zimeimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali. Kwa mfano, kazi yangu ya kucheza mpira wa mezani pia imenufaika. China itatuma makocha wanataaluma Papua New Guinea ili kutoa mwongozo na mafunzo ya kiufundi za tenisi ya mezani. Na mimi pia nimepata fursa ya kuja hapa China kushiriki mafunzo ya mpira wa mezani. Ninatumai siku za baadaye urafiki wa nchi hizo mbili utakuwa wa kina zaidi.”
Geoffrey Loi akihojiwa. (Picha ilipigwa na Peng Yukai/People's Daily Online)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma