BRI ni  Zawadi ya China kwa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2023

Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Jarida la Uongozi la Nigeria Innocent Oddo akihojiwa na waandishi wa habari wa China.(Picha na Aris/Tovuti ya Gazeti la Umma))

Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Jarida la Uongozi la Nigeria Innocent Oddo akihojiwa na waandishi wa habari wa China.(Picha na Aris/Tovuti ya Gazeti la Umma))

Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) unatokana na historia ya kale ya China ya ushirikiano wa kimataifa usio wa unyonyaji na ni zawadi ambayo China imeleta kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi na watu wote.

Kauli hii imesemwa na Innocent Oddo, Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Jarida la Uongozi la Nigeria katika mahojiano na People’s Daily Online kuhusu kujenga kwa pamoja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya China na nchi nyingine duniani.

“Kwakweli ni fursa kubwa kwa nchi yeyote inayoshiriki katika pendekezo hili kwa ajili ya kupata mafanikio yenye kuonekana kwa uhalisia” amesema Oddo ambaye yuko hapa Beijing, China kuhudhuria Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja utakaofunguliwa rasmi kesho Jumanne, Oktoba 17.

“China imeleta zawadi kwa Dunia, tunaweza tu kusonga mbele kutekeleza pendekezo hili” amesema Oddo.

Oddo ameongeza kuwa BRI ni jukwaa muhimu kwa ushirikiano kati ya China na nchi zinazoshiriki, zaidi ya nchi 150 ni washiriki, pia mashirika zaidi ya 130, hivyo ni pendekezo muhimu kwa ajili ya muunganisho, maendeleo ya miundombinu, biashara ya baharini, TEHAMA na sekta nyingine zote ambazo zinatoa uhakikisho wa maendeleo ya binadamu.

Kuhusu muono wake wa baadaye wa pendekezo hilo, Oddo amesema tayari ameanza kuona dalili nzuri.

“Tayari tunaona uwekezaji mpana katika maeneo mengi, ushirikiano wa pande zote na utumiaji wa fursa kwa ajili ya ustawi na manufaa kwa nchi zote duniani. Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja lipo hapa kwa ajili ya kudumu. Litaendelea kuwa bora zaidi na hiki ndicho ninakiona katika siku za baadaye” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha