Kufichua dhana potofu ya nchi za magharibi kuhusu Xinjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2023

Katika miaka ya hivi karibuni, makundi yanayoipinga China ya nchi za Magharibi yametoa dhana potovu mara kwa mara ya "kutumikishwa kwa nguvu", kuipaka matope sura ya China duniani, kufifisha heshima ya China duniani, na kufitinisha uhusiano wa kirafiki kati ya China na nchi nyingine. Profesa Tursun Abai wa Chuo Kikuu cha Xinjiang alifanya uchunguzi zaidi ya habari 30,000 kuhusu Xinjiang zilizotolewa na vyombo 22 vya habari katika nchi na kanda 15 ili kufichua hoja ya uwongo ya ati "kutumikishwa kwa nguvu".

1.Nchi za Magharibi zinalaani kuwapanga na kuwapatia ajira wanafunzi wa kituo cha elimu na mafunzo cha Xinjiang, zikisema kuwa kufanya hivyo ni “kuwatumikisha kwa nguvu”.

Ukweli wa mambo: kuhamisha nguvukazi ya ziada vijijini ni njia muhimu ya serikali ya China ya kuwasaidia wakulima kuongeza mapato. Kutoka mwaka 2014 hadi 2019, mkoani Xinjiang kwa wastani wa kila mwaka, watu waliokuwa nguvukazi ya ziada vijijini waliofika milioni 2.76 walipangwa na kupata ajira katika sehemu nyingine mkoani. Ongezeko la mapato ya matumizi ya watu wa mijini limeongezeka kuwa yuan 34,700 na lile la vijijini limefikia yuan 13,100.

2.Nchi za Magharibi zinaishambulia sera ya China kuhusu Xinjiang ikisema China imefanya dhambi ya " kutokomeza kabila".

Ukweli wa mambo:Chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, idadi ya watu wa kabila la Wauyghur iliongezeka mara 3.2 na kufikia milioni 11.6243 mwaka 2020 kutoka milioni 3.6076 ya mwaka 1953. Katika wakati huo, wastani wa ongezeko la idadi ya watu wa nchi nzima ya China ulikuwa mara 2.4, na ongezeko la idadi ya watu wa kabila la Wauyghur lilikuwa la juu zaidi.

3.Nchi za Magharibi zilishambulia sera ya China kuhusu Xinjiang na kufanya suala la haki za binadamu liwe la kisiasa, kulichukulia kama silaha na nyenzo.

Ukweli wa mambo : China imetoa vitabu 13 vya waraka wa jumla kuhusu haki za binadamu na vitabu 65 vya waraka mbalimbali kuhusu haki za binadamu. Kufikia Aprili 2021, China imealika jumuiya tisa maalum, kama vile Jumuiya ya Watoaji ripoti Maalum kuhusu Uhuru wa uamini dini na Kikundi Kazi cha Kutia mbaroni Kiholela, kutembelea China kwa mara 11. Na tokea mwezi Septemba, 2016, China imefanya mazungumzo karibu 20 kuhusu haki za binadamu kati yake na Umoja wa Ulaya, Uingereza, Ujerumani, Uswizi, New Zealand, Uholanzi na nchi nyingine.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha