Mwandishi habari wa Tanzania: Kanuni ya uwazi ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lavutia zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2023

Tarehe 17 hadi 18 mwezi huu, Baraza la 3 la Ushirikiano wa Kimataifa la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” unafanyika hapa Beijing. Hivi karibuni, mwandishi habari kutoka gazeti la “The Guardian” la Tanzania Mary Kadoke alihojiwa na People’s Daily Online kwenye Kituo cha Vyombo vya Habari cha baraza hilo, ambapo alisema kuwa, kanuni ya uwazi ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” inamvutia zaidi, na sasa ushirikiano kati ya China na Tanzania una mwelekeo mzuri.

Mary alisema, katika kanuni mbalimbali zilizotolewa na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kanuni ya uwazi inamvutia zaidi, aliongeza kuwa ingawa China imepata maendeleo makubwa, ipo tayari kufundisha nchi nyingine teknolojia yake na kuchangia maendeleo ya nchi husika, hii ndiyo maana ya uwazi.

“China ipo tayari kwenda katika nchi nyingine, kuelezea au kuonesha teknolojia iliyo nayo, hii ni jinsi gani wapo tayari kusaidia nchi nyingine” alisema Mary.

Mary ni mmoja kati ya waandishi habari wa ng’ambo alioalikwa kwenye baraza hilo. Kabla ya Mary kuja hapa Beijing, makala yake ilichapishwa kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la “the Guardian”, ambayo imejulisha matunda mbalimbali yaliyopatikana nchini China na Tanzania chini ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Alipoulizwa kuhusu matunda hayo, Mary alisema, aliokumbuka zaidi ni mradi wa daraja la Magufuli. Alisema mradi huo siyo tu utatoa urahisi kwa usafiri wa wakazi wa mkoa wa Mwanza, ambako mradi huo unatekelezwa, na pia unaleta fursa nyingi za ajira.

“Tayari mradi umeshirikisha Watanzania wengi. Nadhani hata baada ya mradi huu kukamilika, Watanzania wengi watanufaika katika eneo la usafiri” alisema Mary.

Tangu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilipotolewa miaka 10 iliyopita, mfumo wa mawasiliano ya watu kati ya China na nchi husika umekamilika zaidi, na sekta ya mawasiliano imepanuliwa. Mary alisimulia hisia yake ya kushiriki kwenye mradi wa mafunzo wa Kituo cha kimatifa cha Mawasiliano ya Uandishi Habari cha China (CIPCC) mwaka huu akisema kuwa, “kupitia mafunzo hayo ninaweza kuunganisha uandishi wangu wa Tanzania na ule wa China, uchanganyiko huo unaninufaika.”

Kutoka miundombinu hadi ushirikiano wa watu, ushirikiano kati ya China na Tanzania umeongeza mambo mengi mapya sambamba na mabadiliko ya wakati. Mary alisema, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili sasa una mwelekeo mzuri . “Ushirikiano wetu ulianzia ujenzi wa reli, lakini sasa umepanuliwa.” Alionesha matarajio juu ya ushirikiano wa “Uchumi wa Buluu (Blue Economy)” uliozungumziwa kwenye mkutano siku hiyo, “nimesikia kwamba hivi sasa China na Tanzania, Kenya na nchi nyingine mbalimbali za Afrika zina miradi husika ya ushirikiano, ninafurahi sana kuona serikali ya China imeweka mikakati mbalimbali ili kuzisaidia nchi husika kufikia maendeleo endelevu.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha