Rais wa China akutana na mwenzake wa Kenya

(CRI Online) Oktoba 19, 2023

Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Kenya William Ruto ambaye yuko ziarani nchini China kuhudhuria mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa “Ukanda Mmoja na Njia Moja”.

Kwenye mazungumzo kati ya viongozi hao, Rais Xi amesema urafiki kati ya China na Kenya umekuwa na historia ndefu. Tangu China na Kenya zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 60 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa zikiheshimiana na kuungana mikono.

Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo zimeshirikiana kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo reli ya SGR ya Nairobi-Mombasa na bandari ya mafuta ya Mombasa, huku ujenzi wa pamoja wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umepata mafanikio nchini Kenya na kuwanufaisha watu wa pande mbili.

Amesema China inauangalia uhusiano kati yake na Kenya kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na iko tayari kushirikiana na Kenya katika kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Rais Ruto amepongeza mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kusema tangu China na Kenya zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 60 iliyopita, pande hizo mbili siku zote zimekuwa zikiaminiana na kuheshimiana.

Hasa tangu Rais Xi alipotoa pendekezo la “Ukanda Moja na Njia Moja”, Kenya imenufaika sana na ushirikiano kati yake na China. Miradi muhimu ikiwemo reli ya SGR ya Nairobi-Mombasa imeinua kwa kiasi kikubwa uwezo wa maendeleo ya kiuchumi ya Kenya na kuwanufaisha watu wake.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha