Rais Xi Jinping wa China akutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2023

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso, ambaye alikuwa Beijing  kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 19. 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso, ambaye alikuwa Beijing kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 19, 2023. (Xinhua/Pang Xinglei)

Beijing - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso siku ya Alhamisi, ambaye alikuwa Beijing kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Akiielezea Jamhuri ya Kongo kama mshiriki mwenye hamasa na mshirika muhimu katika ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, Rais Xi amesema ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili umepata matokeo yanayoonekana.

Amesema kuwa China iko tayari kutafuta fursa na kukuza maeneo mapya ya ushirikiano katika uchumi wa kidijitali na maendeleo ya kijani na Jamhuri ya Kongo, na kukuza ushirikiano wao wa kiwenzi wa kimkakati wa pande zote ili ufikie viwango vipya.

“China inaiunga mkono Jamhuri ya Kongo katika kudumisha uhuru wa nchi, kupinga uingiliaji kati wa nje, na kufanya kazi yake muhimu katika masuala ya kimataifa na kikanda” Rais Xi amesema.

Kwa upande wake Rais Sassou Nguesso amesema kuwa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ni mradi mzuri ambao unaipa dunia mtindo mpya wa maendeleo jumuishi.

Amesema China ni mchangiaji mkubwa wa ukuaji wa uchumi duniani. Jamhuri ya Kongo inatarajia kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na China katika ujenzi wa miundombinu na nishati safi, na kudumisha mawasiliano na uratibu wa karibu ndani ya mifumo kazi ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

“Jamhuri ya Kongo inaunga mkono kikamilifu mapendekezo ya Maendeleo ya Dunia, Usalama wa Dunia na Ustaarabu wa Dunia yaliyopendekezwa na Rais Xi” Rais Sassou Nguesso ameeleza, huku akisema kwamba ni muafaka kwa ajili ya kudumisha ushirikiano wa pande nyingi na haki na usawa wa kimataifa.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso, ambaye alikuwa Beijing  kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 19. 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso, ambaye alikuwa Beijing kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Tatu la Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 19. 2023. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha